Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Serikali Yaanza Mapitio ya Sera ya Watu Wenye Ulemavu
Aug 24, 2023
Serikali Yaanza Mapitio ya Sera ya Watu Wenye Ulemavu
Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Prof. Jamal Katundu akizungumza na wadau wakati wa kikao kazi cha kupitia taarifa ya awali ya mapitio ya Sera ya Maendeleo na Huduma kwa Watu Wenye Ulemavu ya mwaka 2004, kilichofanyika katika Ofisi ya WCF, Kambarage Tower, Jijini Dodoma leo tarehe 24 Agosti, 2023.
Na Na Mwandishi Wetu, DODOMA

Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu imeanza kufanya tathmini na mchakato wa mapitio ya Sera ya Maendeleo na Huduma kwa Watu Wenye Ulemavu ya mwaka 2004 ili kukidhi mahitaji ya sasa.

 

Akifungua kikao cha wadau Agosti 24, 2023 jijini Dodoma cha kupitia taarifa ya awali ya mapitio hayo, Katibu Mkuu wa Ofisi hiyo, Prof. Jamal Katundu, amesema mapitio hayo yanafanywa na serikali kwa kushirikiana na Shirika la Umoja wa Mataifa la Usawa wa Jinsia na Uwezeshaji wa Wanawake (UN WOMEN) huku akitaka yazingatie uwakilishi wa makundi yote ya Watu wenye Ulemavu ili kuwa na sera bora.

 

Baadhi ya wadau wakifuatilia kwa maelezo ya Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Prof. Jamal Katundu (hayupo pichani) wakati wa kikao kazi cha kupitia taarifa ya awali ya mapitio ya Sera ya Maendeleo na Huduma kwa Watu Wenye Ulemavu ya mwaka 2004, Jijini Dodoma tarehe 24 Agosti, 2023. 

 

Naye, Mwakilishi wa UN WOMEN, Jacob Kayombo, amesema shirika limeridhishwa na hatua iliyofikiwa ya mchakato huo na kwamba wanaamini itakamilika kwa wakati.

 

Kwa upande wake, Katibu Mkuu wa Shirikisho la Vyama Vya Watu Wenye Ulemavu (SHIVYAWATA), Jonas Lubago, ameishukuru serikali kwa kutimiza ahadi ya kufanya maboresho ya sera hiyo na kuahidi kushiriki kikamilifu ili kuwa na maboresho mazuri ya sera. 

 

Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Usawa wa Jinsia na Uwezeshaji wa Wanawake (UN WOMEN), Jacob Kayombo akichangia jambo wakati wa kikao hicho.

 

Awali, Mshauri Elekezi ambaye ni Mhadhiri kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Dkt. Consolata Sulley, amesema katika hatua ya awali ya mapitio utafanyika utafiti kwa kupata maoni kutoka kwa wadau ili kuwa na sera bora inayozingatia haki na masuala ya kijinsia kwa Watu wenye Ulemavu.

 

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi