Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Serikali Yaahidi Kulipa Deni la Mifuko ya Hifadhi ya Jamii
May 04, 2018
Na Msemaji Mkuu

Na Frank Mvungi

Serikali imesema ipo tayari kulipa deni la mikopo inayodaiwa na Mifuko ya Hifadhi ya Jamii mara tu baada ya Kanuni za kuunganisha mifuko ya Hifadhi za Jamii kupelekwa kwa wadau ili kupata maoni yao na hatimaye zianze kutumika.

Akizungumza Bungeni Mjini Dodoma, Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Ashatu Kijaji wakati akijibu swali la Mbunge wa Tumbe Mhesimiwa Rashid Ali Abdallah aliyetaka kujua ni lini Serikali itarejesha mikopo kwenye mifuko ya hifadhi ya jamii.

“Mwaka 2016, Serikali ilifanya uhakiki wa deni la Mifuko ya Hifadhi ya Jamii linalotokana na mikopo ya uwekezaji kwenye miradi mbalimbali ili kuandaa utaratibu wa malipo ambapo jumla ya deni lililowasilishwa Serikalini kwa ajili ya uhakiki kwa mifuko yote ni shilingi trilioni 2.1 na deni lililokubalika baada ya uhakiki ni shilingi trilioni 1.2”, alisisitiza Dkt. Kijaji.

Akifafanua, Dkt. Kijaji alisema kuwa baada ya uhakiki kukamilika, Serikali ilianza kuandaa utaratibu wa kulipa deni hilo kwa kutumia hati fungani maalum zilizotarajiwa kuiva katika kipindi cha kati ya miaka mitatu hadi 20.

Alilieleza Bunge kuwa wakati zoezi la kuandaa hati fungani likiendelea, Serikali ililiomba Bunge kuridhia mapendekezo ya Serikali kuunganisha Mifuko ya Pensheni na kuunda mifuko miwili, mmoja kwa ajili ya sekta ya umma na mwingine kwa ajili ya sekta binafsi, hatua ambayo ilisababisha Serikali kusitisha zoezi la kuandaa Hati Fungani maalumu hadi hapo taratibu za kuunganisha Mifuko ya Pensheni zitakapokamilika.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi