Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

JICA Yaahidi Kuendelea Kuimarisha Miundombinu ya Tanzania
Nov 26, 2017
Na Msemaji Mkuu

[caption id="attachment_23471" align="aligncenter" width="750"] Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa (kushoto) akimpongeza Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) Mhandisi Patric Mfugale kwa kupewa Tuzo ya Rais wa JICA mwishoni mwa wiki Jijini Dar es Salaam. Tuzo hiyo imetolewa kwa watu binafsi 23 duniani ikiwa ni kutambua michango yao katika kusimamia miradi ya JICA.[/caption]

Na: Ismail Ngayonga

SERIKALI ya Japan kupitia Shirika la Maendeleo la Kimataifa la nchi hiyo (JICA) imesema itaendelea kuisadia miradi mikubwa ya maendeleo nchini ikiwemo barabara ili kuhakikisha kuwa Tanzania inapiga hatua kubwa katika kuwaletea maendeleo wananchi wake.

Hayo yamesemwa mwishoni wa wiki Jijini Dar es Salaam na Balozi wa Japan nchini, Masaharu Yoshida wakati wa utoaji tuzo ya heshima ya Rais wa JICA kwa Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara Nchini (TANROAD), Mhandisi Patrick Mfugale.

Balozi Yoshida alisema tangu mwaka 1980, JICA imekuwa mshirika wa karibu wa maendeleo na Serikali ya Tanzania ikiwemo kuunga mkono juhudi za kukuza uchumi na kupunguza umasikini kwa wananchi kupitia ufadhili wa miradi ya kipaumbele kwa ikiwemo barabara.

[caption id="attachment_23472" align="aligncenter" width="750"] Balozi wa Japan nchini Mhe. Masaharu Yoshinda (kushoto) akimkabidhi Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) Mhandisi Patric Mfugale Tuzo ya Rais wa JICA mwishoni mwa wiki Jijini Dar es Salaam. Tuzo hiyo imetolewa kwa watu binafsi 23 duniani ikiwa ni kutambua michango yao katika kusimamia miradi ya JICA.[/caption] [caption id="attachment_23473" align="aligncenter" width="750"] wa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) Mhandisi Patric Mfugale kwa mara baada ya kumkabidhi Tuzo ya Rais wa JICA mwishoni mwa wiki Jijini Dar es Salaam. Tuzo hiyo imetolewa kwa watu binafsi 23 duniani ikiwa ni kutambua michango yao katika kusimamia miradi ya JICA.[/caption]

Aliongeza kuwa utoaji wa Tuzo ya Rais wa JICA kwa Mhandisi Mfugale imedhirisha imani ya Serikali ya Japan kwa Tanzania katika kusimamia utekelezaji wa miradi ya maendeleo inayofadhiliwa JICA, na kuahidi kuendelea kuimarisha uhusiano na ushirikiano huo kwa manufaa ya wananchi wa Mataifa hayo.

“Misaada ya JICA nchini unajumuisha misaada bila masharti, misaada ya kiufundi, kufadhili miradi kwenye maeneo ya vipaumbele kwa serikali hususan katika sekta za kilimo, miundombinu ya barabara, maji, nishati, utawala na afya” alisema Balozi Yoshida.

Akizungumzia kuhusu tuzo ya Rais wa JICA kwa Mhandisi Mfugale, Balozi Yoshida alisema tuzo hiyo hutolewa kama alama ya utambuzi wa heshima kwa wataalamu, wataalamu washauri na wafanyakazi wa kujitolea walifanikisha maendeleo katika nyanja za raslimali watu na maendeleo ya miundombinu katika nchi zinazoendelea ikiwemo Tanzania.

[caption id="attachment_23474" align="aligncenter" width="750"] Baadhi ya wafanyakazi wa Shirika la Kimataifa la Maendeleo la Japan (JICA) na Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) wakifutilia hafla ya kumkabidhi Tuzo ya Rais wa JICA Mtendaji Mkuu wa TANROADS Mhandisi Patrick Mfugale mapema wikiendi hii. Tuzo hiyo imetolewa kwa watu binafsi 23 duniani ikiwa ni kutambua michango yao katika kusimamia miradi ya JICA.[/caption] [caption id="attachment_23475" align="aligncenter" width="750"] Mtendaji Mkuu wa TANROADS Mhandisi Patrick Mfugale akionyesha Tuzo ya Rais wa JICA katika hafla ya kukabidhiwa tuzo hiyo mwishoni mwa wiki Jijini Dar es Salaam. Kutoka kulia ni Balozi wa Japan nchini Tanzania Mhe. Masaharu Yoshinda, Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa, Makamu wa Rais wa JICA Hiroshi Kato na Mwakilishi Mkuu wa JICA nchini Tanzania Toshio Nagase.[/caption] [caption id="attachment_23476" align="aligncenter" width="750"] Mtendaji Mkuu wa TANROADS Mhandisi Patrick Mfugale akipokea shada la maua kutoka kwa mmoja wa wafanyakazi wenzake Bi. Beatrice Kosongwa wakati wa hafla ya kumkabidhi Tuzo ya Rais wa JICA iliyofanyika mwishoni mwa wiki Jijini Dar es Salaam. Kutoka kulia ni Balozi wa Japan nchini Tanzania Mhe. Masaharu Yoshinda, Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa, Makamu wa Rais wa JICA Hiroshi Kato na Mwakilishi Mkuu wa JICA nchini Tanzania Toshio Nagase. (Picha na: Frank Shija)[/caption]

Balozi Yoshida alisema tuzo hiyo imetolewa kwa Mhandisi Mfugale kutokana na mchango wake katika maendeleo ya miundombinu inayounganisha mikoa mbalimbali nchini pamoja na nchi jirani na kueneza ujuzi wake kwa wasaidizi waliomzunguka.

Kwa upande wake Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa alisema tuzo ya Mhandisi Mfugale imetoa somo kwa Wahandisi vijana wanaopaswa kuzingatia miiko inayoongoza taaluma ya uhandisi nchini.

Aidha Prof. Mbarawa aliishukuru JICA kwa utekelezaji wa miradi ya barabara nchini hususani katika jitihada zake za kuhakikisha kuwa Tanzania inafikia uchumi wa kati kupitia uimarishaji wa miundombinu imara ya barabara.

“Uadilifu na uaminifu ni jambo la msingi sana katika taaluma ya uhandisi, ni misingi mikuu iliyoonyeshwa katika utendaji kazi Mhandisi Mfugale hadi anatunukiwa tuzo hii, niwahimize wahandisi vijana muige mfano huu” alisema Waziri Mbarawa.

Naye Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROAD), Mhandisi Patrick Mfugale alisema tuzo aliyopewa ni zawadi kwa Serikali hususani wafanyakazi wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano ambao amekuwa akifanya nao kazi  kwa katika kutekeleza majukumu yake.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi