Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Serikali Yawezesha Upatikanaji Huduma bora za Afya  Mkoani Morogoro
Mar 23, 2020
Na Msemaji Mkuu

Na; Mwandishi Wetu

Shilingi Bilioni 4.5 zimetumika kujenga Hospitali za Wilaya mkoani Morogoro ikiwa ni jitihada za Serikali kuhakikisha kuwa huduma za afya zinawafikia wananchi wote.

Akizungumza katika kipindi cha ‘TUNATEKELEZA’ Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Bw.  Loata Ole Sanare amesema kuwa Serikali ya Awamu ya Tano imewezesha wananchi kufikiwa na huduma bora za fya katika maeneo yao.

 “Mkoa wetu kwa sasa una Hospitali za Wilaya katika Wilaya zote baada ya Serikali kutuwezesha kujenga katika Wilaya 3 ambazo hazikuwa na Hospitali za Wilaya”, Alisisitiza Sanare

Akifafanua zaidi, Mhe.  Sanare  amesema kuwa Hospitali hizo zimejengwa katika Wilaya za Malinyi, Morogoro Vijijini na  Gairo  ili kuwezesha wananchi kupata huduma bora za afya.

Aliongeza kuwa dhamira ya Serikali ya kuwawezesha wananchi kupitia huduma bora imeendelea kutekelezwa kupitia ujenzi wa vituo vya afya na zahanati katika Wilaya zote za mkoa huo hivyo kusogeza huduma kwa wananchi.

Aidha,  Serikali imewezesha Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro mjini kujenga soko lenye thamani ya shilingi Bilioni 18 ili kuimarisha upatikanaji wa huduma  kwa wananchi mjini humo na maeneo ya jirani.

Kipindi cha TUNATEKELEZA kinarushwa kila alhamisi kikishirikisha Wakuu wa Mikoa katika awamu hii ili waweze kueleza utekelezaji katika mikoa yao.

   

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi