Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Serikali   Ya Awamu ya Tano Yaendelea Kufanikisha Ujenzi wa Viwanda
May 10, 2018
Na Msemaji Mkuu

Na Frank Mvungi- MAELEZO

Serikali ya Awamu yaTano tangu iingie madarakani imefanikisha Ujenzi wa Viwanda zaidi ya 3306 vikubwa  na Vidogo hadi kufikia machi 2018.

Akiwasilisha Hotuba ya Makadirio ya Mapato na Matumizi,  Waziri wa Viwanda  Biashara na uwekezaji, Mhe. Charles Mwijage amesema kuwa  ujenzi wa viwanda hivyo unatokana na dhamira ya Serikali kujenga uchumi wa viwanda ili kukuza ajira  na uchumi.

“Muongozo wa Kusimamia ujenzi wa Viwanda kwa Tawala za Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa umekamilika’’ Alisisitiza Mwijage

Akifafanua Mhe. Mwijage  amesema kutokana na dhamira safi ya Serikali kujenga uchumi wa Viwanda hali iliyopelekea Tanzania kujitosheleza kwa mahitaji ya nondo, mabati, vinjwaji na vigae.

Katika kufufua viwanda  vilivyosimama kuzalish, Mhe. Mwijage amesema kuwa msimamo wa Serikali nikuhakikisha  kiwanda cha matairi Arusha kinafanya kazi na jukumu la kuboresha na kuendesha kiwanda hicho litakuwa mikononi mwa sekta Binafsi huku Serikali ikibaki na hisa kulingana na rasilimali zilizopo.

Akizungumzia vipaumbele vya Wizara kwa mwaka 2018/19 Mhe. Mwijage amesema kuwa ni kuendeleza miradi ya kielelezo ya Mchuchuma na Liganga, Magadi soda Engaruka na Kiwanda cha Matairi Arusha, Uendelezaji wa eneo la Viwanda TAMCO  Kibaha na mradi wa kuunganisha matrekta.

Vipaumbele Vingine ni uendelezaji wa Mitaa, Maeneo ya Viwanda vya SIDO, Kuendeleza  Kanda  Kuu za Kiuchumi, Ruvuma, Tanga,  Kigoma, Manyoni, Bagamoyo, SZE  na BMSEZ, Kurasini Logistic Centre  na Kigamboni Industrial  Parks.

Aidha ameongeza kuwa, kati ya Julai 2017 hadi Machi 2018 jumla ya miradi 243 yenye thamani ya dola za kimarekani milioni 3,667 imeajiri watu 36,025 na  imesajiliwa na TIC, BRELA  na EPZA.

Vilevile amesema kuwa, tangu  kuanzishwa kwa Mamlaka ya EPZ hadi mwezi machi, 2018 jumla ya mtaji dola bilioni 1.86 uliwekezwa na mauzo ya bidhaa nje ya nchi yamefikia Dola za Kimarekani  milioni 1,359.94 na ajira 52, 698 za moja kwa moja zimepatikana.

Kupitia mradi wa kuunganisha matrekta ya URSUS  ambapo  hadi mwezi Desemba 2017, Semi knocked Down (SKD) za matrekta 2400 yaliyoanishwa katika mkataba wa uunganishaji  unaoendelea.

Pia Wizara itaendeleza tafiti kupitia taasisi zake za TIRDO, CAMARTEC, TEMDO, Dodoma Leather, Dodoma SEZ  na ujenzi wa Indusrial Parks.

Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais Dkt. John Pombe Magufuli imekuwa ikisisitiza umuhimu wa ujenzi wa uchumi wa viwanda kote nchini, Aidha Hotuba ya makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2018/2019.

 

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi