Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Serikali na Wadau Nchini Wafanya Kikao cha Maandalizi
Sep 23, 2018
Na Msemaji Mkuu

[caption id="attachment_35590" align="aligncenter" width="750"] Waziri wa Nishati Dkt Medard Kalemani (kushoto) na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Dkt Adelardus Kilangi (katikati), wakiongoza kikao cha maandalizi kuhusu ushiriki wa Serikali katika Kongamano la Mafuta na Gesi, linalotarajiwa kufanyika jijini Dar es Salaam, Septemba 24 na 25, 2018. Kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Dkt Hamis Mwinyimvua. Kikao hicho kimefanyika leo, Septemba 23, 2018 jijini Dar es Salaam.[/caption]

Na: Veronica Simba – DAR ES SALAAM

Wizara ya Nishati na Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, wameandaa kikao cha maandalizi pamoja na wadau mbalimbali ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya Mkutano mkubwa kuhusu Mafuta na Gesi, unaotarajiwa kufanyika jijini Dar es Salaam, Septemba 24 na 25, mwaka huu.

Akizungumza katika kikao hicho kilichofanyika leo, Septemba 23, 2018 katika Ofisi ndogo za Wizara ya Nishati, jijini Dar es Salaam, Waziri wa Nishati Dkt Medard Kalemani amewaeleza wajumbe kuwa, lengo la Serikali katika Kongamano hilo ni kunadi fursa mbalimbali za uwekezaji zilizopo nchini, hususan katika sekta husika ili kuvutia wawekezaji.

[caption id="attachment_35591" align="aligncenter" width="750"] Waziri wa Nishati Dkt Medard Kalemani (mbele-mwenye shati la bluu) na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Dkt Adelardus Kilangi (kushoto kwa Waziri), wakiongoza kikao cha maandalizi kuhusu ushiriki wa Serikali katika Kongamano la Mafuta na Gesi, linalotarajiwa kufanyika jijini Dar es Salaam, Septemba 24 na 25, 2018. Kikao hicho kimefanyika leo, Septemba 23, 2018 jijini Dar es Salaam.[/caption] [caption id="attachment_35593" align="aligncenter" width="750"] Wawakilishi kutoka Wizara mbalimbali na Taasisi za Serikali, wakiwa katika kikao cha maandalizi kuhusu ushiriki wa Serikali katika Kongamano la Mafuta na Gesi, linalotarajiwa kufanyika jijini Dar es Salaam, Septemba 24 na 25, 2018. Kikao hicho kimefanyika leo, Septemba 23, 2018 jijini Dar es Salaam na kimeongozwa na Waziri wa Nishati Dkt Medard Kalemani na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Dkt Adelardus Kilangi (hawapo pichani)[/caption]

“Tulitumie kongamano hili kama fursa kwetu kuelezea nafasi mbalimbali za uwekezaji tulizo nazo katika sekta husika.”

Katika kikao hicho, wajumbe wamejadili namna gani wataweza kuiwakilisha Serikali vyema kupitia ushiriki wao katika kongamano hilo.

Kikao kimehusisha wawakilishi mbalimbali kutoka Wizara ya Nishati; Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji; Ardhi, Maji, Nishati na Mazingira-Zanzibar; Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu; Katiba na Sheria; Fedha na Mipango; Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki; Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano pamoja na Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi.

Aidha, wawakilishi kutoka Taasisi mbalimbali za Serikali wameshiriki pia kikao hicho. Taasisi hizo ni pamoja na Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), Pangea Securities, EPZA, Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA), Mamlaka ya Udhibiti wa Mkondo wa Juu wa Petroli (PURA), Mamlaka ya Udhibiti wa Petroli (ZPRA), Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) pamoja na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi