Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Serikali Kutenga Bajeti kwa Ajili ya Uzalishaji wa Pamba Mbegu Vipara – Bashungwa
Mar 01, 2019
Na Msemaji Mkuu

Naibu Waziri wa Kilimo Mhe Innocent Bashungwa (Mb) akisisitiza jambo wakati akizungumza kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika kijiji cha Muhunze kilichopo katika Wilaya ya Kishapu wakati wa ziara ya Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan Mkoani Shinyanga leo tarehe 28 Februari 2019.

Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Shinyanga

Serikali imeeleza kuwa imejipanga kuimarisha zao la Pamba ili kuongeza uzalishaji nchini kwani kufanya hivyo wakulima watanufaika katika uzalishaji wenye tija na kuimarisha biashara.

Ili kuongeza uzalishaji wa Pamba dhamira ya serikali ni kuanzisha Pamba mbegu vipara ili kuondokana na utumiaji wa pamba manyoya ambayo imezoeleka lakini tija yake ni ndogo katika uzalishaji kuliko Pamba Manyonya.

Naibu Waziri wa Kilimo ameyasema hayo leo tarehe 28 Februari 2019 wakati akizungumza kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika kijiji cha Muhunze kilichopo katika Wilaya ya Kishapu wakati wa ziara ya Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan Mkoani Shinyanga.

Baadhi ya wananchi wakifatilia mkutano wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan wakati akizungumza kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika kijiji cha Muhunze kilichopo katika Wilaya ya Kishapu wakati wa ziara ya kikazi Mkoani Shinyanga leo tarehe 28 Februari 2019.

Alisema kuwa elimu itatolewa kuhusu matumizi ya Pamba mbegu vipara ili kuwajengea uelewa wananchi na serikali kufikia hatua ya kufungamanisha kilimo cha Pamba na uchumi wa viwanda.

Mhe Bashungwa aliongeza kuwa serikali ya awamu ya tano  inayoongozwa na Mhe Rais Dkt JKohn Pombe Magufuli imejipanga kuhakikisha kuwa kilimo kinawakomboa wananchi ili kuimarisha uchumi wa mtu mmoja mmoja na Taifa kwa ujumla wake.

“Sisi kama Wizara tutakuwa na jukumu la kushawishi wawezaji ili kuwekeza kwenye viwanda vya Pamba nyuzi pamoja na viwanda vya nguo na kufanya hivyo tutakuwa tumetekeleza vyema maelekezo yaliyoainishwa kwenye ilani ya Uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi yam waka 2015-2020” Alikaririwa

Naibu Waziri wa ardhi, Nyumba na Maendeleo ya makazi Dkt Angeline Mabula  (Mb) akisisitiza jambo wakati akizungumza kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika kijiji cha Muhunze kilichopo katika Wilaya ya Kishapu wakati wa ziara ya Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan Mkoani Shinyanga leo tarehe 28 Februari 2019.
Kutoka kushoto ni Naibu Waziri wa Tawala za mikoa na serikali za mitaa TAMISEM Mhe Mwita Waitara, Naibu Waziri wa Kilimo Mhe Innocent Bashungwa (Mb), Naibu Waziri wa Madini Mhe Stanslaus Nyongo wakifatilia mkutano wa hadhara uliofanyika katika kijiji cha Muhunze kilichopo katika Wilaya ya Kishapu wakati wa ziara ya Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan Mkoani Shinyanga leo tarehe 28 Februari 2019.
Aidha, alisema kuwa Wizara ya Kilimo imejipanga vyema katika kutafuta masoko ya mazao ya wakulima ambapo kwa upande wa zao la mahindi tayari soko limepatikana kupitia Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) imesaini mkataba wa mauziano ya mahindi ya Tani 36,000 na Mpango wa Chakula Duniani (WFP).
 
Katika hatua nyingine alisema kuwa wakulima wa Wilaya ya Kishapu ni miongoni mwa wakulima wa zao la Mtama hivyo kupitia Mpango wa Chakula Duniani (WFP) serikali ya Tanzania inaendelea kujiridhisha uhitaji wa mtama nchini Sudani Kusini ili kuwaunganuisha wakulima na soko hilo.
 
Katika hatua nyingine Naibu Waziri huyo ameiagiza Bodi ya Pamba kuhakikisha viuadudu (Viuatifu) vinapatika haraka katika Wilaya ya  kishapu ili kuondoa haraka changamoto inayowakumba wakulima kwa kukosekana viuatilifu kwa wakati.
 
 

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi