Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Serikali Kukamilisha Ujenzi wa Nyumba 5,000 Msomera Ndani ya Miezi Sita
Oct 17, 2023
Serikali Kukamilisha Ujenzi wa Nyumba 5,000 Msomera Ndani ya Miezi Sita
Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taif,a Mheshimiwa Dkt. Stergomena Tax akiongea na Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mheshimiwa Geophrey Pinda wakati wa kukagua maendeleo ya ujenzi wa nyumba 5,000 za wakazi wa Msomera wilayani Handeni mkoa wa Tanga.
Na Hassan Mabuye, Handeni Tanga

Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Mheshimiwa Dkt. Stergomena Tax amesema Serikali inatarajia kukamilisha ujenzi wa nyumba 5,000 ambazo zimeanza kujengwa za Wakazi wa Msomera wilayani Handeni, Mkoa wa Tanga waliohama kwa hiari kutoka Hifadhi ya Taifa ya Ngorongoro.

 

Dkt. Tax ameyasema hayo wakati alipofanya ziara ya kutembelea maendeleo ya ujenzi wa nyumba hizo zinazojengwa katika Kijiji cha Msomera mkoani Tanga akiongozana na Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mheshimiwa Geophrey Pinda.

"Lengo letu ni kuhakikisha kwamba nyumba 1,000 zinakamilika mwishoni mwa mwezi Oktoba 2023 na tutaendelea kuzikabidhi nyumba kadri zinavyokwisha, lakini nyumba 5,000 zinarajiwa kukamilishwa mwishoni mwa mwezi Machi 2024" Dkt. Tax amesema.

 

"Kama mnavyoona hii ni oparesheni inayofanywa na Jeshi la Wananchi la Tanzania (JWTZ) hususan Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) ambapo ujenzi huu unahusisha sekta nyingi na ndio maana nimeongozana na Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleeo ya Makazi na sekta nyingine za Nishati na Maji ili kufanya haraka kwa wakazi hawa kupata malazi ya kudumu". Aliongeza Dkt. Tax.

 

Naye Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mheshimiwa Geophrey Pinda amesema Wizara yake ndio ya mwanzo kabisa katika utekelezaji wa mradi huu kwani ndio inafanya maandalizi ya kupanga na kupima ardhi ili sekta nyingine zianze kufanya kazi kikamilifu.

"Wizara yetu ndio ya kwanza kabisa kufika eneo hili kuja ambapo ilikuja kulitambua eneo hili la msomera tangu lilipotolewa agizo la kuwaandalia makazi wananchi wa eneo hili, hivyo tumefanikiwa kulipanga na kulipima japo bado baadhi ya maeneo tunaendelea kuyapanga na kutatua migogoro ya mipaka". Alisema Pinda.

 

Pinda amesisitiza kwamba Wizara yake itaendelea kushirikiana kwa karibu na Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa na taasisi nyingine katika kuharakisha ukamilishaji wa operesheni hiyo.

Katika kukamilisha kazi hii, Pinda ameahidi kukutana na viongozi wa Wilaya ya Simanjiro na Kilindi wenye mgogoro wa mipaka ya Wilaya na Wilaya ili kutatua mgogoro huo unaokwamisha zoezi la kupanga makazi ya wananchi hao.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi