Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Serikali Kuendeleza Ushirikiano na ILO Katika Programu za Ajira Kwa Vijana
Oct 27, 2018
Na Msemaji Mkuu

[caption id="attachment_37497" align="aligncenter" width="1000"] Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akizungumza na wajumbe wa shirika Kazi Duniani (ILO) na watendaji wakuu wa Idara na Vitengo kutoka Ofisi yake walipokutana kujadili kuhusu programu za shirika hilo hii leo Oktoba 27, 2018 Bungeni Jijini Dodoma.[/caption]

Na: Mwandishi Wetu

Serikali kuendeleza ushirikiano na Shirika la Kazi Duniani (ILO) katika kuendeleza programu na mipango mbalimbali hususan kwenye masuala ya kazi nchini.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama  ameyasema hayo alipokutana na kufanya  majadiliano na wajumbe wa shirika hilo na watendaji wakuu wa Idara na Vitengo kutoka Ofisi yake walipokutana hii leo Oktoba 27, 2018 Bungeni Jijini Dodoma.

[caption id="attachment_37498" align="aligncenter" width="1000"] Mkurugenzi wa Shirika la Kazi Duniani Kanda ya Afrika Mashariki, Bw. Wallington Chibebe akifafanua jambo kuhusu programu za ILO kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama na watendaji wakuu wa Idara na Vitengo kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu (hawapo pichani). (Kulia) ni Mwandamizi wa Programu za ILO, Bw. Anthony Rutabanzibwa.[/caption] [caption id="attachment_37499" align="aligncenter" width="1000"] Baadhi ya wajumbe kutoka Shirika la Kazi Duniani (ILO) wakimsikiliza Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama (hayupo pichani) walipokutana kujadili kuhusu programu za shirika hilo leo Oktoba 27, 2018.[/caption]

Akizungumza wakati wa mkutano huo Waziri Mhagama alisema kuwa zipo programu ambazo zinafanyiwa kazi na ILO kwa kushirikiana na Serikali kwenye masuala ya maendeleo ya ajira kwa vijana, ikiwemo kuwajengea ujuzi ambao utawasaidia kujiajiri au kuunganishwa kwenye masoko ya ajira ambayo tunayo hapa nchini.

"Programu hizi zitakuwa ni chachu katika kutatua masuala mbalimbali na kuleta maendeleo ambayo yatafanikisha mipango ya serikali," alisema Mhagama.

Aidha, aliongeza kuwa programu hizo zitawajumuisha vilevile watu wenye ulemavu kwa kuwapatia mafunzo ya ujuzi na stadi za kazi kupitia programu hizo.

[caption id="attachment_37500" align="aligncenter" width="1000"] Kamishna wa Kazi Bw. Gabriel Malata (wa kwanza kushoto) akichangia mada wakati wa mkutano huo.[/caption]

Katika hatua nyingine kikao hiko kimekubaliana kuanzisha kamati ya pamoja ambayo itaangalia programu za ILO namna ambavyo zinaweza kuuwiana na programu za Serikali.

Mhe. Mhagama  alilishukuru shirika hilo kwa mchango wake katika kusaidia masuala mbali mbali ikiwemo  programu ya Taifa ya Kazi za Staha, ukuzaji ujuzi, programu ya kuhamasisha uwekezaji wenye kuzalisha fursa za ajira, mapitio ya sera za kinga ya jamii na ajira, uridhiaji wa mikataba ya viwango vya kazi vya kimataifa, maandalizi ya mkakati wa kutokomeza ajira mbaya kwa watoto na mkakati wa kutokomeza maambukizi ya virusi vya ukimwi maeneo ya kazi.

[caption id="attachment_37501" align="aligncenter" width="1000"] Sehemu ya Watendaji Wakuu wa Idara na Vitengo kutoka Ofisi ya Waziri MKuu wakifuatilia maelezo ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama walipokutana Jijini Dodoma.[/caption] [caption id="attachment_37502" align="aligncenter" width="750"] Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama (wa tano kutoka kulia) akiwa kwenye picha ya pamoja na wajumbe wa shirika Kazi Duniani (ILO) na watendaji wakuu wa Idara na Vitengo kutoka Ofisi yake walipokutana leo Oktoba 27, 2018 Bungeni Jijini Dodoma.[/caption]

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Shirika la Kazi Duniani Kanda ya Afrika Mashariki, Bw. Wallington Chibebe alisema kuwa ILO itaendeleza programu hizo kwa kuzingatia vipaumbele vya Serikali ambazo ni pamoja na kuendeleza mafunzo ya kazi za uanagenzi zitawawezesha vijana kujiajiri.

“Ushirikiano ndio jambo muhimu katika kutekeleza majukumu tuliopanga  kwa faida ya kuimarisha maendeleo ya jamii kwa ujumla,” alisema Chibebe.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi