[caption id="attachment_36283" align="aligncenter" width="900"] Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Tume ya Taifa ya Kudhibiti Ukimwi (TACAIDS) Jumanne Issanga akifungua mkutano wa wadau uliolenga kujadili maboresho yanayopaswa kufanywa ili kuongeza ubora wa namna ya kupambana na janga la Ukimwi hapa nchini hasa kwa kuangalia sheria mbalimbali zinazosimamia suala la ukimwi na pia kuweka mikakati bora itakayowezesha kutolewa kwa huduma bora kwa waathirika waliopo katika makundi maalum Jijini Dodoma kwa siku mbili kuanzia leo Oktoba 3,2018.[/caption]
Na: Frank Mvungi
Wadau kutoka katika Taasisi mbalimbali hapa nchini wamekutana Jijini Dodoma kujadili na kuweka mikakati ya pamoja na kupitia sheria mbalimbali zinazosimamia mapambano dhidi ya ukimwi ili kuongeza tija katika huduma zinazotolewa.
Akizungumza wakati akifungua mkutano huo wa wadau Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Kudhibiti Ukimwi (TACAIDS) Bw. Jumanne Issanga amesema kuwa dhamira ya mkutano huo ni kupitia sheria mbalimbali zilizopo na ambazo zinasimamia mapambano dhidi ya ukimwi hapa nchini ili kuona mapungufu yaliyopo na kuweka mikakati ya pamoja yakusaidia katika kuongeza mapambano hayo na kuboresha sheria zilizopo.
[caption id="attachment_36284" align="aligncenter" width="900"]"Tumekutana na wadau hapa Dodoma kujadili kwa pamoja na kuona namna gani tunakuja na mkakati wa pamoja unaotokana na mkutano huu ili tungeze tija katika huduma zinazotolewa kwa waathirika na hasa walio katika makundi maalum" Alisisitiza Issanga
Akifafanua amesema kuwa maazimio yatakayotokana na kikao hicho yatasaidia Serikali katika kuhakikisha kuwa janga hili linapigwa vita na kila mtanzania na hivyo kufikiwa kwa malengo ya kutokomeza janga hili.
Kwa upande wake Mwanasheria wa Tume hiyo Mwanasheria wa Tume ya Taifa ya Kudhibiti Ukimwi (TACAIDS) Bw. Miraji Mambo amesema kuwa wadau wanaoshiriki katika mkutano huo wanatoka katika Taasisi za Jeshi la Magereza, Jeshi la Polisi,NACOFA,TAMISEMI, Wizara ya Afya na wadau wengine wanaoshiriki katika mapambano dhidi ya Ukimwi hapa nchini.
[caption id="attachment_36286" align="aligncenter" width="900"]"Kwa pamoja kwa muda wa siku mbili tunaamini tutapitia sheria mbalimbali na kuona mapungufu yaliyopo ili tutoe mapendekezo ya namna bora ya kuendeleza mapambano haya dhidi ya janga la Ukimwi na hatimaye kufikiwa kwa malengo"; Alisisitiza Mambo
Aliongeza kuwa kuna umuhimu mkubwa kwa wadau kukutana na kuangali kwa pamoja namna bora ya kufanya mapambano dhidi ya janga hilo yafanikiwe.
Kwa upande wake Mratibu wa Ukimwi TACAIDS mkoa wa Tanga Bw. Juma Mbilinyi amesema kuwa kuna haja kwa jamii kuongeza mwamko wa kupima na kujua hali ili kuchukua hatua stahiki .
Matokeo ya tafiti zilizofanyika yanaonesha kuwa kuna haja kwa kila mwanajamii kushiriki kikamilifu katika mapambano dhidi ya janga la ukimwi.