Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Serikali Kuendelea Kufuta Milki Mashamba Yaliyotelekezwa
Nov 07, 2018
Na Msemaji Mkuu

[caption id="attachment_37817" align="aligncenter" width="750"] Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Angellina Mabula akijibu swali wakati wa kikao cha pili cha Mkutano wa 13 wa Bunge leo jijini Dodoma.[/caption]

Na: Beatrice Lyimo

Serikali imeendelea kuchukua hatua za kubatilisha milki za ardhi za mashamba yaliyotekelezwa katika maeneo mbalimbali nchini.

Hayo yamesema Bungeni leo  na Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Angelina Mabula  wakati akijibu swali la Mhe. Dustan Kitandula Mbunge wa Mkinga kuhusu kufuta hati za mashamba yaliyotelekezwa.

"Katika kipindi cha Disemba, 2015 mpaka Octoba, 2018 mashamba yenye ukubwa wa ekari 84,240.803 yamebatilishwa katika Halmashauri za Ngorongoro, Arumeru, Moshi, Kinondoni,(Manispaa), Kigamboni(Manispaa), Mvomero, Kilombero, Kilosa, Mvomero, Iringa, Bukoba, Tarime, Kibaha, Serengeti, Busega, Muheza, Lushoto na Mkinga" amefafanua Naibu Waziri Mabula.

Mabula anasema kuwa, katika Halmashauri ya Wilaya ya Mkinga, Shamba Na. 278 Mkomazi lenye ukubwa wa ekari 15,442 lililokuwa likimilikiwa na kampuni ya M/S Mkomazi Plantations Limited kwa Hati Namba 4268, 9780  na 9781 milki yake ilithibitishwa tarehe 20 Juni, 2018.

Aidha anafafanua kuwa, baada ya kubatilishwa kwa milki ya shamba hilo, Serikali ya Mkoa wa Tanga kwa kushirikiana na Halmashauri ya Wilaya ya Mkinga zipange matumizi mapya ya shamba hilo kwa kuzingatia mahitaji ya ardhi katika eneo hilo kipaumbele kikiwa ni mahitaji ya wananchi na ardhi kwa ajili ya uwekezaji.

Mbali na hayo Mabula amezitaka Halmashauri zote nchini kubaini mashamba yaliyotelekezwa kutuma ilani kwa wamiliki wa mashamba hayo kwa mujibu wa Sheria ya Ardhi (Sura 113) na kuwasilisha mapendekezo katika Wizara ya Ardhi kwa hatua za kubatilisha milki za mashamba hayo ziweze kufanyika.

 

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi