Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Serikali Itaendelea Kuweka Mkazo Michezo Yote - Mwinjuma
Oct 30, 2023
Serikali Itaendelea Kuweka Mkazo Michezo Yote - Mwinjuma
Naibu Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Hamis Mwinjuma akiwa katika picha Oktoba 29 2023 wilayani Kilombero mkoani Morogoro wakati akifunga mashindano ya Gofu ya Kilombero Open yaliyoambatana na ugawaji wa zawadi kwa washindi.
Na Mwandishi Wetu

Naibu Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Hamis Mwinjuma amesema Serikali itaendelea kuweka mkazo kwenye michezo ya aina zote katika ngazi zote kwa kuwa michezo ni ajira, biashara na uchumi.

Mhe. Mwinjuma ameyasema hayo Oktoba 29 2023 wilayani Kilombero mkoani Morogoro wakati akifunga mashindano ya Gofu ya Kilombero Open yaliyoambatana na ugawaji wa zawadi kwa washindi.

"Sisi wasaidizi wa Mhe. Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan kazi yetu ni kutekeleza kwa vitendo maono yake na moja ya shughuli tulizopewa ni kuhakikisha mkazo unawekwa sio kwenye mchezo mmoja lakini kwenye michezo yote na kwenye ngazi zote mpaka chini, jana nilifunga ligi kwenye kata inaitwa Mwaya kule Ulanga, unaweza kuona nimeenda kwenye mashindano ya jimbo ya mpira wa miguu na Netiboli na leo niko hapa, yote ni kutekeleza maono ya Mhe. Rais ya kwamba tuweke mkazo na tuhakikishe kwamba kila mchezo kwenye ngazi yoyote jicho la Serikali linakuwepo," amesisitiza Mhe. Mwinjuma

Mhe. Mwinjuma amekiomba  Kiwanda cha Sukari Kilombero licha ya kuwekeza kwenye mpira wa gofu  kiwekeze pia kwenye mpira wa miguu kwa kuwa na timu ya mpira wa miguu ili vijana waendelee kunufaika na Michezo.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi