Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Serikali Itaendelea Kumuenzi Marehemu Membe - Majaliwa
Aug 26, 2023
Serikali Itaendelea Kumuenzi Marehemu Membe - Majaliwa
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiweka shada la maua kwenye kaburi la marehemu Bernard Membe baada ya kushiriki Ibada ya Kumbukumbu ya marehemu Bernard Membe iliyofanyika nyumbani kwa marehemu kijijini Londo katika Halmashauri ya Mtama mkoani Lindi, Agosti, 26, 2023.
Na Mwandishi Wetu

Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa amesema Serikali itaendelea kuyaenzi mambo yote mazuri yaliyofanywa na Marehemu, Bernad Membe wakati wa Utumishi wake Serikalini.

Ameyasema hayo leo Agosti 26, 2023 aliposhiriki ibada ya kumbukumbu ya marehemu Membe iliyofanyika nyumbani kwa marehemu Rondo, Lindi.

Marehemu Membe ambaye aliwahi kuwa Waziri wa Mambo ya Nje alifariki dunia Mei 12 mwaka huu katika Hospitali ya Kairuki jijini Dar es Salaam alikokuwa akipatiwa matibabu.

Amesema Marehemu Membe enzi za uhai wake alikuwa mwanadiplomasia mahiri kwenye medani za Kitaifa na Kimataifa, hivyo Serikali na Watanzania wataendelea kumkumbuka.

Mhe. Majaliwa amesema weledi, nidhamu, uchapakazi na umahiri wa marehemu Membe uliitambulisha Tanzania katika medani za kimataifa na kutengeneza marafiki na mataifa mengine.

“Mheshimiwa Membe alikuwa na weledi wa kitaifa na kimataifa, jumuiya za kimataifa zinatambua umahiri wake  na alijizolea sifa kwa sababu ya nidhamu na uchapakazi wake", alisema Mhe. Majaliwa.

Naye, Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Nape Nnauye akizungumza kwa niaba ya familia ya marehemu aliishukuru Serikali kwa ushirikiano ilioutoa katika kipindi cha msiba.

“Namshukuru Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutoa zaidi ya shilingi milioni 100 kwa ajili ya ukarabati wa kanisa ulioanzishwa na Marehemu Membe. “

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi