Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Serikali inatambua Mchango wa Machifu katika Kulinda Mila na Desturi za Nchi.
May 28, 2019
Na Msemaji Mkuu

[caption id="attachment_43599" align="aligncenter" width="1000"] Naibu Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe.Juliana Shonza(kulia) akizungumza na Machifu kutoka Mkoa wa Singida na Mara Wilaya ya Rorya ambao walimtembelea ofisini kwake leo Mei 28 Jijini Dodoma kujadili masuala mbalimbali yanayohusu namna ya kuendeleza na kuhifadhi Mila na Desturi za nchi yetu.[/caption]

Na Shamimu Nyaki- WHUSM

Naibu Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe.Juliana Shonza amesema kuwa Serikali inatambua mchango na jitihada kubwa zinazofanywa na Machifu wa makabila mbalimbali ya Tanzania katika kuhifadhi,kulinda na kuendeleza Mila na Desturi za Taifa hili.

Mhe.Shonza ameyasema hayo leo Jijini Dodoma wakati alipofanya Kikao na Machifu wa Mkoa wa Singida pamoja na Rorya waliofika ofisini kwake kujadili mambo mbalimbali yanayohusu Sekta ya Utamaduni ambapo amewaeleza kuwa wao kama viongozi wenye dhamana ya kuendeleza mila na desturi za makabila yao ni jukumu lao kuhakikisha kuwa wanafanya kazi hiyo kwa lengo la kuutangaza Utamaduni wa nchi yetu.

[caption id="attachment_43600" align="aligncenter" width="1000"] Mkurugenzi Idara ya Mendeleo ya Utamaduni Wizara ya Habari,Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt. Emmanuel Temu akizungumza katika kikao cha Naibu Waziri Mhe Juliana Shonza (wa pili kulia) pamoja na Machifu wa Singida na Rorya kilichokua na lengo la kujadili namna ya kuendeleza na kuhifadhi Mila na Desturi za nchi yetu kilichofanyika leo Mei 28,Jijini Dodoma.[/caption] [caption id="attachment_43601" align="aligncenter" width="1000"] Chifu Ngoja Ongabo wa Rorya (katikati) akieleza jambo katika kikao cha Naibu Waziri Mhe Juliana Shonza (hayupo katika picha) pamoja na Machifu wa Singida na Rorya kilichokua na lengo la kujadili namna ya kuendeleza na kuhifadhi Mila na Desturi za nchi yetu kilichofanyika leo Mei 28,Jijini Dodoma.[/caption]

"Serikali inatambua juhudi mnazofanya katika kuendeleza Mila na Desturi za maeneo yenu ndio maana imetenga maeneo ambayo mnakutana kufanya shughuli za kiutamaduni ikiwemo kuandaa mfumo rasmi wa kuwatambua"alisema Mhe.Shonza.

Aidha amewataka machifu hao kushirikiana na Maafisa Utamaduni wa Mikoa na Halmashauri wakati wanapotaka  kufanya shughuli za kiutamaduni katika maeneo yao.

Kwa upande wake  Chifu wa Rorya Bw.Ngoja Ongabo ameishauri Serikali kutoa ushirikiano kwa Machifu katika Wazo lao la kuanzisha Baraza la Wazee ambalo litasaidia kuwaunganisha Wazee wa makabila mbalimbali yaliyopo hapa nchini na kujadili namna bora ya kuhifadhi mila na Desturi zetu.

Naye Chifu Omary Hamis wa Singida ameiomba Serikali kuweka mipaka katika maeneo ya kufanyia shughuli za utamaduni ili kuepuka migogoro ya ardhi inayotokana na wanachi kuvamia maeneo hayo.

Hata hivyo Serikali imepokea ushauri uliotolewa na machifu hao ambapo imeahidi kuzifanyia kazi.

[caption id="attachment_43602" align="aligncenter" width="1000"] Naibu Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe.Juliana Shonza(kulia) akisikiliza na kuandika mchango wa Bw.Iddi Juma Ndabu kutoka Singida wakati alipofanya kikao na Machifu kutoka Mkoa wa Singida na Mara Wilaya ya Rorya ambao walimtembelea ofisini kwake leo Mei 28 Jijini Dodoma kujadili masuala mbalimbali yanayohusu namna ya kuendeleza na kuhifadhi Mila na Desturi za nchi yetu.[/caption]

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi