Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Serikali Imewataka Watanzania Kuenzi Utamaduni Kwani ni Sehemu ya Utalii
Oct 10, 2018
Na Msemaji Mkuu

[caption id="attachment_36596" align="aligncenter" width="1000"] Wacheza ngoma kutoka jamii ya Wasonjo Kutoka Ngorongoro wakicheza ngoma ya asili wakati wa ufunguzi wa Tamasha la Urithi Festival leo katika uwanja wa Shekhe Amri Abed Jijini Arusha ambapo mgeni rasmi wa ufunguzi wa tamasha hilo alikuwa Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Bi.Susan Mlawi (hayupo pichani).[/caption]

Na Anitha Jonas – WHUSM

Serikali imewataka watanzania kudumisha  na kurithisha amali za urithi wa asili wa utamaduni wa kitanzania kwa vijana na watoto kwa manufaa ya kizazi kijacho.

Kauli hiyo imetolewa leo jijini Arusha na Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Bi. Susan Mlawi alipokuwa akifungua Tamasha la Urithi Festival kwa niaba ya Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Utamaduni Dkt. Harrison Mwakyembe katika uwanja wa Shekhe Amri Abed.

Akiendelea kuzungumza katika  sherehe hizo za ufunguzi wa Tamasha hilo Bi.Mlawi asisitiza kuwa uwepo wa tamasha hilo utatoa fursa mbalimbali kwa watanzania wa kunadi,kuonesha na kutangaza rasilimali za  utalii wa utamaduni  ndani na nje ya nchi.

“Uanuai wa Maendeleo ya sekta ya utalii wa kiutamaduni ili uishi na usiwe katika hatari ya kupotea unahitajika kutambua na kuthamini urithi wa Jadi kama Mila,Desturi,Lugha,Maadii na Imani hivyo uhifadhi,utafiti na utasaidia kunadi kutaendeleza rasilimali za asili za taifa,”alisema Bi.Mlawi.

[caption id="attachment_36597" align="aligncenter" width="1000"] Mama kutoka jamii ya Kimeru Bi.Sophia Pallangyo akimwonyesha mgeni rasmi ambaye ni Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Bi.Susan Mlawi (hayupo pichani) namna jamii hiyo ilivyokuwa ikitumia mawe kusaga mahindi kupata unga kama sehemu ya maonesho ya zana za asili,wakati mgeni rasmi alipombelea banda hilo leo katika Maonesho ya washiriki wa Tamasha la Urithi Festival linalofanyika uwanja wa Shekhe Amri Abed Jijini Arusha.[/caption]

Kwa upande wa Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Tamasha la Urithi Festival Taifa Prof.Audax Mabula alieleza kuwa wazo la kuanzishwa kwa tamasha hilo lilitokea Wizara ya Maliasili na Utalii lengo likiwa ni kutangaza utalii wa kiutamaduni kwani Tanzania imebarikiwa kuwa na vivutio vingi vya kiutamaduni ambavyo ni hazina kuwa kwa Taifa.

“Nchi yetu imebarikiwa kwa kuwa na vivutio vingi vya kiutamaduni kama michoro ya mapangoni inayopatika kama Kondoa,makundi manne ya lugha za afrika yanayopatikana mkoa wa Manyara na jirani,ngoma za asili kutoka makabila mbalimbali nchini pamoja na vyakula vya asili,”alisema Prof.Mabula.

[caption id="attachment_36599" align="aligncenter" width="1000"] Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Bi.Susan Mlawi akitizama namna maziwa yanahifadhiwa kwenye kibuyu na Bi Neema Mollel. Kutoka jamii ya Kimasai alipotembelea banda la wanawake kimasai wakati wa ufunguzi wa Tamasha la Urithi Festival uliyofanyika leo jijini Arusha katika uwanja wa Shekhe Amri Abed.[/caption] [caption id="attachment_36600" align="aligncenter" width="1000"] Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Bi.Susan Mlawi wapili kushoto akipata maelezo ya vyakula asili kwa Bi.Marium alipotembelea banda la kabila la Warangi leo katika uwanja wa Shekhe Amri Abed jijini Arusha katika ufunguzi wa Tamasha la Urithi Festival.[/caption] [caption id="attachment_36602" align="aligncenter" width="1000"] Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Bi.Susan Mlawi akiwata watanzania kuenzi vya kula vya asili,mila nzuri,desturi na lugha za asili kwa lengo la kutangaza utalii wa kiutamaduni wa taifa katika ufunguzi wa Tamasha la Urithi Festival leo jijini Arusha katika uwanja wa Shekhe Amri Abed.[/caption] Aidha, nae Mkurugenzi Mkuu  Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyapori Tanzania Dkt. James Wakibala  alitoa salamu za Waziri wa Maliasili Utamaduni Sanaa na Michezo kwa wadau wa Mkoa wa Arusha na viongozi wake waliyoshiriki tamasha hilo kwa kuwapongeza katika kushiriki tamasha hilo ambalo kwa namna moja litasaidia kuendeleza utalii katika sekta ya Utamaduni. Hata hIvyo Katibu Mkuu huyo katika hitimisho la hotuba yake aliiomba Wizara hiyo ya Maliasili na Utalii kushirikiana na Wizara yake katika maandalizi ya tamasha hilo kwa mwakani kwani wote wanadhamana ya kukuza  na kutangaza utalii wa Kiutamaduni. Halikadhalika hitimisho la Tamasha hilo kwa mwaka huu linatarajiwa kufanyika Oktoba 13,mkoani hapo na Waziri Mkuu wa Tanzania Mhe.Kassim Majaliwa.    

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi