Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Serikali Imewataka Wadhibiti Ubora wa Elimu Kutekeleza Majukumu yao Kwa Weledi
Jul 19, 2018
Na Msemaji Mkuu

[caption id="attachment_33757" align="aligncenter" width="900"] Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako akisisitiza umuhimu wa kutumia kwa malengo yaliyokusudiwa magari 45 yaliyotolewa na Serikali kwa wadhibiti ubora wa Elimu ngazi ya Kanda na Wilaya leo Jijini Dodoma wakati wa Hafla ya kukabidhi magari hayo ikiwa ni sehemu ya juhudi za Serikali kuboresha elimu hapa nchini.katika hafla hiyo Baraza la Mitihani Tanzania nalo lilipatiwa magari 2 na kufanya jumla ya magari yaliyotolewa kuwa 47.[/caption]

Frank Mvungi- MAELEZO, Dodoma

Serikali imewataka Wadhibiti Ubora wa Elimu katika ngazi zote kutekeleleza majukumu yao kwa weledi ili kukuza kiwango cha elimu hapa nchini.

Akizungumza leo Jijini Dodoma wakati wa hafla ya kukabidhi magari 47 kwa wadhibiti Ubora wa Elimu na Baraza la Mitihani (NECTA), Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Joyce Ndalichako amesema ku ni utekelezaji wa sehemu ya mikakakti ya kukuza elimu hapa nchini hasa kipindi hiki Taifa linapoelekea katika ujenzi wa uchumi wa viwanda.

Kati ya hayo, 45 yamekabidhiwa kwa wadhibiti ubora wa elimu ngazi ya Kanda na Wilaya na 2 kwa Baraza la Mitihani Tanzania (NECTA) .

[caption id="attachment_33758" align="aligncenter" width="900"] Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako akiendesha moja ya magari yaliyotolewa na Serikali kwa wadhibiti ubora wa Elimu ngazi ya Kanda na Wilaya leo Jijini kama sehemu ya kuzindua na kukabidhi magari hayo.[/caption]  

"Imani yangu ni kuwa magari haya yatatunzwa vizuri na yatatumika kufanya kazi na malengo yaliyokusudiwa na si vinginevyo hivyo yatasaidia kuboresha elimu hapa nchini " Alisisitiza Prof. Ndalichako

Akifafanua, Prof. Ndalichako  amesema kuwa magari hayo yanalenga kusaidia Taifa kuzalisha wataalamu wenye weledi, mahiri na wabunifu hasa katika kipindi hiki Taifa linapoelekea katika ujenzi wa uchumi wa viwanda.

[caption id="attachment_33759" align="aligncenter" width="900"] Sehemu ya magari 47 yalitolewa na Serikali ambapo wadhibiti ubora wa elimu ngazi ya Kanda na Wilaya wamekabidhiwa magari 45 na mawili yamekabidhiwa Baraza la Mitihani Tanzania (NECTA).[/caption]

Aliongeza kuwa Serikali haitasita kuwachukulia hatua kali wale wote watakaotumia magari hayo kwa maslahi binafsi na wale watakaoshindwa kutimiza wajibu wao kwa mujibu wa sheria na kanuni zinazosimamia sekta ya elimu.

Katika kuimarisha elimu, Prof. Ndalichako amesema kuwa Serikali imefungua ofisi mpya 5 za udhibiti ubora wa shule katika Halmashuri za Songwe, Kigambaoni, Ubungo, Chalinze na Ushetu kwa lengo la kuimarisha shughuli za udhibiti ubora katika Halmashuri.

Jambo jingine ni kuandaliwa kwa mkakati wa Taifa wa Elimu jumuishi (2018-2021) ili kushughulikia masuala ya elimu kwa watoto wote wakiwemo wenye mahitaji maalum na kutoa fursa kwa wadau wengine wa maendeleo kupata maeneo ya kuchangia utekelezaji  wa elimu jumuishi.

[caption id="attachment_33760" align="aligncenter" width="900"] Sehemu ya washiriki wa hafla ya kukabidhiwa magari 47 , ambapo kati ya magari hayo 45 yamekabidhiwa kwa wadhibiti ubora wa elimu ngazi ya Kanda na Wilaya na 2 yamekabidhiwa Baraza la Mitihani Tanzania (NECTA).[/caption]

Hivi karibuni Serikali kupitia Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia ilikabidhi pikipiki 2,894 ambazo zimesambazwa katika halmashuri 156 katika mikoa 25, pikipiki hizo zitasaidia waratibu elimu kata katika kutekeleza majukumu yao ili kuhakikisha kuwa elimu bora inatolewa shuleni katika maeneo yao.

Magari 45 yaliyotolewa kwa Wadhibiti ubora wa elimu ngazi ya kanda na wilaya na 2 kwa Baraza la Mitihani Tanzania (NECTA) ni chachu katika kuimarisha sekta ya elimu  hapa nchini na kuongeza ari kwa watendaji katika sekta ya elimu.

[caption id="attachment_33761" align="aligncenter" width="900"] Magari yalikabidhiwa kwa wadhibiti ubora wa elimu ngazi ya Kanda na Wilaya yakiondoka katika viwanja wa Chuo Kikuu Dodoma baada ya hafla ya makabidhiano iliyofanyika leo Jijini Dodoma ambapo Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako alikuwa mgeni rasmi.[/caption] Mwanafunzi Bora wa Kidato cha sita kwa masomo ya Sanaa, ambaye ameshika nafasi ya pili Kitaifa kutoka shule ya Sekondari Mvumi Dodoma Bw. Erick Maximillian akizungumzia siri yakufanikiwa kushika nafasi hiyo wakati wa hafla kukabidhi magari 47 , ambapo kati ya magari hayo 45 yamekabidhiwa kwa wadhibiti ubora wa elimu ngazi ya Kanda na Wilaya na 2 yamekabidhiwa Baraza la Mitihani Tanzania (NECTA). [caption id="attachment_33762" align="aligncenter" width="900"] Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako akimpongeza Bw. Erick Maximillian ambaye ni mwanafunzi Bora wa masomo ya Sanaa nafasi ya pili Kitaifa kutoka shule ya Sekondari Mvumi Dodoma wakati wa hafla kukabidhi magari 47 , ambapo kati ya magari hayo 45 yamekabidhiwa kwa wadhibiti ubora wa elimu ngazi ya Kanda na Wilaya na 2 yamekabidhiwa Baraza la Mitihani Tanzania (NECTA).[/caption] [caption id="attachment_33763" align="aligncenter" width="900"] Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia Dkt. Ave Maria Semakafu akizungumza wakati wa hafla ya ya kukabidhiwa magari 47 , ambapo kati ya magari hayo 45 yamekabidhiwa kwa wadhibiti ubora wa elimu ngazi ya Kanda na Wilaya na 2 yamekabidhiwa Baraza la Mitihani Tanzania (NECTA).[/caption] [caption id="attachment_33764" align="aligncenter" width="900"] Mkurugenzi wa Uthibiti Ubora Kutoka Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia Bi Ufrasia Buchuma akitoa neno la shukrani kwa Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako mara baada ya hafla ya kukabidhiwa magari 47 , ambapo kati ya magari hayo 45 yamekabidhiwa kwa wadhibiti ubora wa elimu ngazi ya Kanda na Wilaya na 2 yamekabidhiwa Baraza la Mitihani Tanzania (NECTA).[/caption] [caption id="attachment_33756" align="aligncenter" width="900"] Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu Prof. James Mdoe akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhiwa magari 47 , ambapo kati ya magari hayo 45 yamekabidhiwa kwa wadhibiti ubora wa elimu ngazi ya Kanda na Wilaya na 2 yamekabidhiwa Baraza la Mitihani Tanzania (NECTA). (Picha zote na Frank Mvungi- MAELEZO)[/caption]        

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi