Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Serikali Haitaivunja TEWW Kwa Kuwa Bado Inahitajika
Feb 09, 2018
Na Msemaji Mkuu

[caption id="" align="aligncenter" width="750"] Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako akionesha kwa wabunge baadhi ya Vitabu vyenye ubora unaotakiwa kwa matumizi ya wanafunzi ikiwa ni moja ya hatua zilizochukuliwa na Serikali katika kuimarisha elimu nchini ambapo pia alibainisha kuwa Serikali haitaivunja Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima badala yake inaangalia namna bora yakuimarisha Taasisi hiyo.[/caption]   [caption id="attachment_28734" align="aligncenter" width="750"] Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako akisisitiza jambo kwa wabunge wakati akijibu hoja za Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii Bungeni Mjini Dodoma.[/caption]

Na Mwandishi  Wetu

 Serikali imesema iko tayari kupokea ushauri wa namna bora yakuimarisha utendaji wa Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima (TEWW) kwa kuwa azma ya Serikali ni kuendeleza Taasisi hiyo kwani bado inahitajika na madhumuni ya kuanzishwa kwake  yana  tija kwa Taifa.

Akizungumza wakati akijibu Hoja za Wabunge na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii, Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Profesa. Joyce Ndalichako amesema kuwa Bado Taasisi hiyo inahitajika hivyo Serikali inaangalia namna ya kuiboresha na si kuivunja kama ilivyopendekezwa.

“Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima ilianzishwa kwa lengo la kutoa elimu kwa wale waliokosa elimu katika mfumo rasmi na pia kutoa mafunzo  endelevu hivyo bado kuna umuhimu wa kuiendeleza Taasisi hii” Alisisitiza Prof. Ndalichako.

Akifafanua, Prof. Ndalichako amesema kuwa Taasisi hiyo inaweza kuimarishwa zaidi ili kuendana na mahitaji ya sasa ikiwa ni sehemu ya mikakati ya Serikali kuimarisha na kukuza kiwango cha elimu nchini.

Akizungumzia mikakati yakuimarisha elimu nchini Profesa Ndalichako amesema kuwa kwa sasa Serikali inafanya ukarabati wa Shule Kongwe hapa nchini, vyuo vya Ualimu, na Ujenzi wa maktaba ya kisasa katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam yenye uwezo wa kuchukua wanafunzi zaidi ya 2500 kwa wakati mmoja ikiwa ni sehemu ya miradi yakuboresha elimu inayotekelezwa na Serikali ya Awamu ya Tano.

Maoni ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii yalipendekeza kuwa TEWW ivunjwe ambapo Serikali imesema Bado Taasisi hiyo inahitajika na ina tija hivyo kitakachofanyika ni kuiboresha zaidi ili kukuza elimu hapa nchini na Si kuivunja kama ilivyopendekezwa.

Taasisi hiyo imeanzishwa kwa sheria namba 139 ya mwaka 1989 na iko chini ya Wizara ya Elimu Sayansi na Teknoloji.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi