Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Sekta Binafsi Ziko Tayari Kushirikiana Na Serikali Kujenga Makazi Bora
Mar 23, 2022
Na Jacquiline Mrisho

Na Mwandishi Wetu - MAELEZO

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amesema sekta binafsi ziko tayari kuunga mkono juhudi za serikali za kuboresha makazi na nyumba za wananchi.

Mhe. Rais Samia ameyasema hayo leo (Machi 23, 2022) katika hafla ya uzinduzi wa nyumba 644 za makazi za Magomeni Kota zilizopo jijini Dar es Salaam.

“Sekta binafsi wako tayari kushirikiana nanyi Wakala wa Majengo Tanzania (TBA), wako tayari kushirikiana nanyi na kujenga maeneo yote mtakayosema yanahitaji kujengwa.

“Jambo la maana hapa ni kukaa vyema na kufanya mijadala na kukubaliana mikataba yenye tija baina yenu na sekta binafsi,” amearifu Rais Samia.

Sambamba na hilo, Mkuu wa Nchi ameuagiza uongozi wa TBA, Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) na Watumishi Housing kukaa na sekta binafsi ya ndani au nje ya nchi na kukubaliana kuendeleza maeneo yote ambayo yako wazi na yanayopaswa kuendelezwa.

“Kwa sababu tukisema yaendelezwe na serikali itatuchukua muda mrefu lakini sekta binafsi wako tayari kutoa hizo fedha,” amehabarisha Rais Samia.

Pamoja na hilo, Mhe. Rais amesema mahitaji ya nyumba bora yanakadiriwa kuwa zaidi ya milioni tatu na kwamba takriban nyumba laki mbili zinakisiwa kuongezeka kwa kila mwaka.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi