Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

SAMIA- Tunahitaji Kufanya Mambo Makubwa Sekta ya Afya EAC
Mar 28, 2019
Na Msemaji Mkuu

[caption id="attachment_41464" align="aligncenter" width="1000"] Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia wakati wa ufunguzi wa Kongamano la 7 la Afya na Sayansi la Afrika Mashariki lililofanyika katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)[/caption]

Na. Paschal Dotto

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amefungua mkutano wa  Teknolojia na Utafiti wa Sayansi ya Afya kwa nchini wanachama wa Jumuiya ya Afrika ya Mashariki na Kuzindua Mifumo na teknoljia ya kidijitali itakayotumika kutoa huduma za Afya kwa nchi wanachama leo jijini, Dar es Salaam.

Akizungumza katika Hafla hiyo ya ufunguzi, Mama Suluhu amesema mifumo hiyo mitatu ambayo ni Digital REACH Initiative Strategic Plan 2019-2028, The East Africa Web Portal for Heath Informations  na YEARS Forum itachochea utaoaji wa huduma za afya kwa wanachi wa Afrika Mashariki.

“Mkutano wetu leo umekusanyisha wadau wote wa sekta ya afya Afrika Mashariki, lakini pia wataalam wengine kutoka kwengineko duniani, na dhumuni ni kuweza kuangalia matumizi ya teknolojia katika kuboresha na kutatua changamoto za huduma za afya kidijitali zaidi”,  alisema Makamu wa Rais.

[caption id="attachment_41465" align="aligncenter" width="1000"] Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwasha mwenge kama ishara ya ufunguzi wa Kongamano la 7 la Afya na Sayansi la Afrika Mashariki lililofanyika katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)[/caption]

Aidha, Mama Suluhu alisema kuwa mkutano utatoa fursa kwa nchi wanachama wa Jumuiya hiyo kubadilishana mawazo ili kuweza kuipanua kwa kasi sekta ya afya katika ukanda wa Afrika Masharikia, kwa kuwa uchumi wa sasa ni uchumi wa kati, unaohitaji watu wenye afya bora katika kufanya kazi, kwa hiyo kunahitajika kuwepo na huduma za afya za uhakika na kwa haraka zaidi kwa kutumia teknolojia ya kisasa zaidi.

 Naye Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu alisema kuwa  Mkutano huu wa  siku tatu unajumuisha wanasayansi watafiti na watoa huduma za afya kutoka EAC na nje, ambao watatoa tafiti na Mada za tafiti za kina, ambazo zitawapa Mawaziri fursa ya kupata uzoefu katika kuboresha sera na kuja na maamuzi katika kuboresha huduma za afya.

“Rwanda wanatumia ndege isiyo na rubani katika kusambaza dawa, chanjo na damu katika kukabiliana na vifo vya mama wajawazito katika maeneo ya vijijini, kadhalika badala ya kutumia makaratasi katika hospitali, na kwa vile wananchi wengi wana simu, tumeanza kuhakikisha tunatumia teknolojia katika utoaji wa huduma za afya ili kukabiliana na changamoto, ikiwemo ya kupotea kwa mafaili na kupata taarifa za msaada wa huduma za afya kutoka hospitali moja hadi nyingine nchni”, alisema Waziri wa Afya.

[caption id="attachment_41466" align="aligncenter" width="1000"] Sehemu ya Wataalamu waliohudhuria ufunguzi wa Kongamano la 7 la Afya na Sayansi la Afrika Mashariki lililofanyika katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)[/caption]

Waziri Ummy alisema kuwa katika mkutano huo, Tanzania watapata maarifa katika matumizi ya teknoljia na kuongeza uhakika wa matumizi hayo, alitoa mfano wa  Hospitali ya Taifa Muhimbili kuwa  tangu waanze kutumia teknolojia katika kuhifadhi taarifa, kupotea kwa mafaili kumepungua kwa asilimia 40-60, baada ya kuwaasa watoa huduma kutumia teknolojia.

“Tutaendelea kuhimiza watoa huduma watumie zaidi teknolojia mbalimbali katika kuboresha utoaji wa huduma za afya, madaktari bingwa wa masuala ya uzazi kwa  wanawake wameanzisha mtandao wa WhatsApp ambapo iwapo kunachangamoto katika utoaji wao wa huduma, basi wanawasiliana na kupeana msaada/ushauri  na hii  imeweza kutusaidia ndani ya miezi mitatu, kwani  imeokoa vifo sita tangu ianzishwe”, Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu.

 

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi