Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Ripoti ya Takwimu za Mazingira Yatajwa Kuwa ya Kihistoria
Oct 18, 2018
Na Msemaji Mkuu

  [caption id="attachment_37005" align="aligncenter" width="900"] Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira Mhe. Mussa Sima akizungumza na washiriki wa hafla ya uzinduzi wa Ripoti ya Taifa ya Takwimu za Mazingira ya mwaka 2017 leo Jijini Dodoma kwa niaba ya Waziri wa  nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba.[/caption]

Na; Mwandishi wetu

Ripoti ya Taifa ya Takwimu za Mazingira ya mwaka 2017 iliyozinduliwa leo Jijini Dodoma imetajwa kuwa ya kihistoria na itasaidia Serikali katika kuchukua hatua stahiki kupambana na uharibifu wa mazingira.

Akizungumza kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, Naibu Waziri wa Ofisi hiyo Mhe. Mussa Sima (Mb) wakati akizindua ripoti hiyo leo Jijini Dodoma amesema kuwa ripoti hiyo ni ya kuhistoria na itasaidia katika kuchukua hatua mbalimbali kukabiliana na uharibifu wa mazingira hapa nchini.

Matokeo yanaonesha kuwa kuna upotevu wa misitu takribani hekta 372,000 tangu mwaka 1995 hadi 2010 hivyo ni muhimu kuchukua hatua stahiki kuondokana na changamoto za uharibifu wa mazingira”. Alisisitiza Mhe. Sima.

[caption id="attachment_37006" align="aligncenter" width="843"] Naibu Waziri, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira Mhe. Mussa Sima akikata utepe kuzindua Ripoti ya Taifa ya Takwimu za Mazingira ya mwaka 2017 leo Jijini Dodoma kwa niaba ya Waziri wan chi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba.[/caption]

Akifafanua amesema kuwa ripoti hiyo inaonesha kuwa miji 10 tu ndio yenye miundo mbinu ya maji taka ambayo inanufaisha wananchi takribani asilimia 10.

Aliongeza kuwa Serikali imejipanga kikamilifu kukabiliana na changamoto za uharibifu wa Mazingira kwanza kwa kuweka mfumo wa kisheria unaosimamia suala hilo na pia kuweka Taasisi mahususi inayosimamia masuala yote ya mazingira hapa nchini.

Pia alitoa wito kwa Wizara na Idara zinazojitegemea kutenga Bajeti kwa ajili ya vitendea kazi,uchakataji wa takwimu za mazingira katika maeneo yao ili kushiriki kikamilifu katika kutunza mazingira na kuchochea maendeleo endelevu yanayoenda sambamba na utunzaji wa mazingira.

Aliongeza kuwa Serikali kwa kuthamini umuhimu wa uwekezaji imeweka mazingira mazuri yanayowawezesha wawekezaji kupata cheti cha Tathmini ya mazingira ndani ya siku 70 kutoka siku 149 za awali ili kuharakisha mchakato wa uwekezaji na kuvutia wawekezaji.

[caption id="attachment_37007" align="aligncenter" width="900"] Mtakwimu mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) Bw. Pius Kasikana akiwasilisha mada wakati wa hafla ya kuzindua Ripoti ya Taifa ya Takwimu za Mazingira ya mwaka 2017 leo Jijini Dodoma.[/caption]

Pia aliwataka Wakuu wa Mikoa na Wilaya kutenga maeneo ya uwekezaji  na kuyapima ili wawekezaji wanapojitokeza wapatiwe maeneo hayo yakiwa yamepimwa ili kuharakisha maendeleo.

Uzinduzi wa Ripoti ya Takwimu za Mazingira ya mwaka 2017 ni kichocheo cha maendeleo kwa kuwa inatoa taswira halisi ya hatua zinazopaswa kuchukuliwa ili kulinda mazingira na kutekeleza miradi yote kwa kuzingatia sheria ya mazingira ya mwaka 2004 na Kanuni zake.

[caption id="attachment_37008" align="aligncenter" width="900"] Naibu Waziri, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira Mhe. Mussa Sima akionesha Ripoti ya Taifa ya Takwimu za Mazingira ya mwaka 2017 leo Jijini Dodoma mara baada yakuizindua leo Jijini Dodoma.[/caption] [caption id="attachment_37009" align="aligncenter" width="790"] Naibu Waziri, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira Mhe. Mussa Sima akimkabidhi Ripoti ya Taifa ya Takwimu za Mazingira ya mwaka 2017 Mkurugenzi wa Shughuli za Kitakwimu Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) Bw. Irenius Ruyobya leo Jijini Dodoma.[/caption] [caption id="attachment_37010" align="aligncenter" width="900"] Meneja wa Takwimu za Bei na Ajira Bi Ruth Minja akiwasilisha mada wakati wa hafla ya kuzindua Ripoti ya Taifa ya Takwimu za Mazingira ya mwaka 2017 leo Jijini Dodoma.[/caption] [caption id="attachment_37004" align="aligncenter" width="900"] . Mhadhiri wa Chuo Kikuu Ardhi Dkt. Anes Mahenge akiwasilisha mada wakati wa uzinduzi wa Ripoti ya Taifa ya Takwimu za Mazingira ya mwaka 2017 leo Jijini Dodoma.
                                                                                      (Picha zote na Frank Mvungi- MAELEZO)[/caption]

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi