Na Tiganya Vincent- RS Tabora.
Mkuu wa mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri amewataka Wakuu wa wilaya, Wakurugenzi na wakuu wa Idara za Halmashauri zote za mkoa huo kutoa elimu ya usafi wa mazingira pamoja na matumizi sahihi ya vyandarua vyenye viuatilifu vya muda mrefu ili kukabiliana na ugonjwa wa malaria.
Bw. Mwanri alitoa wito huo jana mjini Tabora wakati akifungua mkutano wa siku moja kwa viongozi mbalimbali mkoani humo kuhusu mpango endelevu wa ugawaji wa vyandarua vyenye viuatilifu vya muda mrefu kupitia vituo vya kutolewa huduma za afya na shule za msingi.
Alisema kuwa elimu sahihi itasaidia wananchi kuacha kutumia vyandarua kwa matumizi mengine badala ya kujikinga na mbu ili kupunguza vifo vinavyotokana na ugonjwa na malaria .
Mkuu huyo Mkoa aliongeza wananchi wakifahamu juu ya usafi wa mazingira utasaidia kuondoa mazalia mbu katika makazi yao.
Kwa upande wa Katibu Tawala Mkoa wa Tabora Dkt. Thea Ntara alitoa wito kwa watalaam kusaidia mkakati wa kuangamiza kabisa mazalia ya mbu kama sehemu ya kuondoa ugonjwa wa malaria hapa nchini.
Aidha , Katibu Tawala huyo wa Mkoa wa Tabora aliiomba jamii kubadirika na kuanza kutumia vyandarua vyenye viuatilifu ili kuokoa maisha ya Mama na mtoto.
Naye Mganga Mkuu wa Mkoa wa Tabora Dkt. Gunini Kamba alisema mpango wa kugawa vyandarua katika vituo vya kutoa huduma za afya ,shule za msingi na katika ngazi ya familia unakusudia kupunguza maambukizi ya maralia hapa nchini.
Aliongeza kuwa vyandarua hivyo vitasaidia kupunguza maambukizi ya ugonjwa wa malaria mkoani hapa kutoka asilimia 19.5 ya sasa na kushuka zaidi