Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

RC Geita Atoa Ahadi kwa Msemaji Mkuu wa Serikali na Viongozi wa TAGCO
Sep 27, 2018
Na Msemaji Mkuu

[caption id="" align="aligncenter" width="1000"] Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhandisi Gabriel Robert akiongea katika kikao Kilichowahusisha Wakuu wa Wilaya, wakurugenzi wa Halmashari, Viongozi wa Chama cha Maafisa Mawasiliano Serikalini (TAGCO) na Maafisa Habari katika Mkoa wa Geita na Kumhakikishia Msemaji Mkuu wa Serikali na Viongozi wa TAGCO kuwa Mkoa utafanya mageuzi katika sekta ya habari ikiwamo kuwanunulia vifaa muhimu maafisa Habari katika Mkoa wa Geita.[/caption]

Na Mwandishi wetu-MAELEZO GEITA Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhe. Robert Gabriel ameahidi kufanya mageuzi makubwa katika sekta ya habari katika Mkoa wake ili kuhakikisha taarifa za mkoa huo zinawafikia watanzania. Akiongea wakati wa kikao kilichowakutanisha Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi wa Halmashari katika Mkoa wa Geita Mhandisi Gabriel amesema kuwa Mkoa unatekeleza miradi mingi ya maendeleo hivyo ili kuweza kuwafikia wananchi ataviwezesha vitengo vya mawasiliano ili viweze kutekeleza jukumu hilo “Nawaahidi Viongozi wa TAGCO na Msemaji Mkuu wa Serikali nitawanunulia vifaa vyote muhimu Maafisa Habari katika Mkoa wa Geita, wanipe mahitaji yao najua nitakapopata fedha tutavinunua hivyo vifaa vyote ili kuweka mazingira mazuri ya kuwahabarisha watanzania, Serikali inatekeleza hivyo lazima watanzania wajue”-Alisema Mhandisi Robert

Mkurugenzi wa Idara ya Habari-MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi akiongea na Wakuu wa Wilaya na wakurugenzi wa Halmashari katika Mkoa wa Geita na kuwasisiitiza umuhimu wa kuitumia kada ya habari katika kufikisha taarifa kwa wananchi juu ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo

[caption id="attachment_35733" align="aligncenter" width="1000"] Mwenyekiti wa Chama cha Maafisa Mawasiliano Serikalini (TAGCO) Bw. Pascal Shelutete akiongea na Wakuu wa Wilaya na wakurugenzi wa Halmashari na kuwahakikishia viongozi hao kuwa Maafisa Mawasiliano Serikalini watatumia Taaluma yao kuwafikia wananchi na kuwaeleza yale yanayotekelezwa na Serikali.[/caption]  

Akiongea wakati wa Semina elekezi kwa Wakuu wa Wilaya na wakurugenzi wa Halmashari katika Mkoa wa Geita Mkurugenzi wa Idara ya Habari-MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi amewaeleza viongozi hao umuhimu wa kufikisha taarifa kwa wananchi juu ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo na kuwataka kuwashirikisha Maafisa Habari kwenye vikao vya kawaida vya maamuzi ili wawe Maafisa Habari wenye Habari Aidha Dkt. Abbasi alisisitiza Kuwa ni muhimu kwa viongozi wa Serikali kuwekeza katika Mitandao ya kijamii kwani huko ndio dunia ilipo kwa sasa. Naye Mwenyekiti wa Chama cha Maafisa Mawasiliano (TAGCO) Bw. Pascal Shelutete watahakikisha Maafisa Mawasiliano Serikalini Wanatumia Taaluma yao kuwafikia wananchi na kuwaeleza yale yanayotekelezwa na Serikali. “Makandarasi wako kazini wanatengeneza madaraja, wengine wanatengeneza reli ya kisasa hivyo kama ilivyo wao na sisi tutaingia kazini na kuhakikisha tunatumia taaluma yetu vizuri lengo ni kuieleza jamii mambo makubwa mazuri yanayotekelezwa na Serikali ya awamu ya tano Katibu Tawala Mkoa wa Geita aliwataka Wakuu wa Wilaya na wakurugenzi wa Halmashari kufanya vikao vya kila mara ili kupeana mrejesho wa kile kinachofanyika katika mkoa ikiwemo utekelezaji wa Miradi

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi