Rais Samia Suluhu Hassan Azindua Mfumo wa Usafirishaji wa Dharura kwa Wajawazito na Watoto Wachanga M-MAMA Jijini Dodoma
Apr 06, 2022
Na
Jacquiline Mrisho
Viongozi mbalimbali pamoja na Wananchi wa Mkoa wa Dodoma wakiwa katika viwanja vya Chinangali Park Jijini Dodoma kuhudhuria hafla ya uzinduzi wa Mfumo wa usafirishaji wa dharura kwa Wajawazito na Watoto wachanga M-MAMA uliofanywa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan leo tarehe 06 Aprili, 2022.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akimsikiliza Mkurugenzi wa M-MAMA, Bi. Dolorosa Duncan kuhusu Mfumo wa usafirishaji wa dharura kwa Wajawazito na Watoto wachanga M-MAMA kabla ya kuuzindua katika hafla iliyofanyika Viwanja vya Chinangali Park Jijini Dodoma leo tarehe 06 Aprili, 2022.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akibonyeza Kitufe kuzindua Mfumo wa usafirishaji wa dharura kwa Wajawazito na Watoto wachanga M-MAMA katika hafla iliyofanyika Viwanja vya Chinangali Park Jijini Dodoma leo tarehe 06 Aprili, 2022.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akimpongeza Msanii Christian Bella kwenye uzinduzi wa Mfumo wa usafirishaji wa dharura kwa Wajawazito na Watoto wachanga M-MAMA katika hafla iliyofanyika Viwanja vya Chinangali Park Jijini Dodoma leo tarehe 06 Aprili, 2022.
Mkururugenzi wa Idara ya Habari - MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali, Bw. Gerson Msigwa akizungumza jambo na Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Nape Nnauye, Naibu Waziri wa Wizara hiyo, Mha. Kundo Mathew na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dkt. Jim Yonazi wakati wa uzinduzi wa Mfumo wa usafirishaji wa dharura kwa wajawazito na watoto wachanga (M-MAMA) katika hafla iliyofanyika Viwanja vya Chinangali Park leo Jijini Dodoma
Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Nape Nnauye akizungumza jambo na Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom, Sitholizwe Mdlalose na Mkuu wa Idara ya Uhusiano na Mawasiliano Vodacom Group, Mwamvita Makamba wakati wa uzinduzi wa Mfumo wa usafirishaji wa dharura kwa wajawazito na watoto wachanga (M-MAMA) katika hafla iliyofanyika Viwanja vya Chinangali Park leo Jijini Dodoma.