Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Rais Samia Suluhu Hassan ahutubia katika Jubilee ya miaka 25 ya Utumishi wa Uaskofu wa Askofu wa Jimbo Katoliki la Rulenge Ngara.
Feb 22, 2022
Na Jacquiline Mrisho


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia viongozi mbalimbali wa dini katika Sherehe za kumpongeza Askofu wa Jimbo Katoliki la Rulenge Ngara, Severine Niwemugizi katika Jubilee ya Miaka 25 ya Utumishi wake wa Uaskofu leo tarehe 22 Februari, 2022 katika viwanja vya Posta Ngara mkoani Kagera.
 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Askofu wa Jimbo Katoliki la Rulenge Ngara, Severine Niwemugizi mara baada ya kuwasili katika viwanja vya Posta Ngara kwa ajili ya kuhudhuria Sherehe za kumpongeza Askofu huyo leo tarehe 22 Februari, 2022
 

Sehemu ya Viongozi mbalimbali wa Dini, Mapadree, Masista, pamoja na wananchi wa Ngara wakiwa katika Jubilee ya miaka 25 ya Askofu wa Jimbo Katoliki la Rulenge Ngara, Severine Niwemugizi iliyofanyika katika viwanja vya Posta Ngara mkoani Kagera.

Shamrashamra za Jubilee ya Miaka 25 ya Askofu wa Jimbo Katoliki la Rulenge Ngara, Severine Niwemugizi katika viwanja vya Posta Ngara mkoani Kagera.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa katika picha na Askofu wa Jimbo Katoliki la Rulenge Ngara, Severine Niwemugizi, viongozi mbalimbali wa Serikali na Watoto wa kipapa wa Jimbo Katoliki la Rulenge Ngara katika Jubilee ya Miaka 25 ya Utumishi wake wa Uaskofu leo tarehe 22 Februari, 2022 katika viwanja vya Posta Ngara mkoani Kagera.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa katika picha na Askofu wa Jimbo Katoliki la Rulenge Ngara, Severine Niwemugizi, pamoja na Maaskofu wengine kutoka majimbo mbalimbali Katoliki nchini, na nje ya nchi katika Jubilee ya Miaka 25 ya Utumishi wake wa Uaskofu leo tarehe 22 Februari, 2022 katika viwanja vya Posta Ngara mkoani Kagera.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi