Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Rais Samia Mgeni Rasmi Siku ya Kiswahili Duniani
Jun 29, 2022
Na Jacquiline Mrisho

Na Shamimu Nyaki

Rais wa Jamhuri ya  Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuwa Mgeni Rasmi katika Maadhimisho ya Siku ya Kiswahili Duniani yatakayofanyika kitaifa Julai 07, 2022  jijini Dar es Salaam

Akizungumza na Waandishi wa Habari leo Juni 29, 2022, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe. Amos Makalla amesema kuwa, analishukuru Shirika la UNESCO nchini kwa kuendelea  kuipa heshima lugha ya Kiswahili kwa kuadhimisha siku hiyo maalum kila Julai 7 ya kila mwaka.

"Maadhimisho haya kwa mwaka huu ni ya kipekee sana, tunatarajia kupata wageni wengi mashuhuri kutoka ndani na nje ya nchi, akiwemo Rais Mstaafu wa Msumbiji, Mhe. Joachim Chisano, Rais Mstaafu wa Namibia, Mhe. Sam Nujoma, hii ni heshima kubwa kwa mkoa wetu", alisema Mhe. Makalla.

Ameongeza kwa kueleza kuwa, maadhimsho hayo yatahusisha shughuli mbalimbali ikiwemo  kongamano  kuhusu mchango wa lugha ya Kiswahili katika Harakati za Ukombozi wa Bara la Afrika,  litakalofanyika  Julai 06, 2022  ambapo  Balozi Mstaafu, Mhe. Ame Mpungwe ataongoza mada mbalimbali.

Maadhimisho hayo yatatanguliwa na Tamasha la Utamaduni la Kwanza Kitaifa ambalo litafanyika katika Uwanja wa Uhuru kuanzia Julai 01 hadi 03, 2022.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi