Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Rais Samia Azindua Mitambo ya Uchorongaji Madini ya Wachimbaji Wadogo
Oct 21, 2023
Rais Samia Azindua Mitambo ya Uchorongaji Madini ya Wachimbaji Wadogo
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akibonyeza Kitufe kuashiria uzinduzi wa Mitambo ya Uchorongaji kwa ajili ya Wachimbaji wadogo na Mitambo ya Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) kwenye hafla iliyofanyika kwenye ukumbi wa Jakaya Kikwete Jijini Dodoma tarehe 21 Oktoba, 2023.
Na Mwandishi Wetu

Rais wa Jamhuri ya Muungano  wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan  leo Oktoba 21, 2023 amezindua  Mitambo 5 ya Uchorongaji kwa ajili ya wachimbaji wadogo pamoja na vifaa kazi vingine vya Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) vyenye jumla ya thamani ya shilingi 9,178,559,128.

Uzinduzi huo umefanyika katika Kituo cha Mkutano cha Jakaya Kikwete jijini Dodoma  ambapo umeenda sambamba na kukabidhi vifaa hivyo kwa wachimbaji  wadogo wakiwemo Shirikisho la Wachimbaji Wadogo Tanzania (FEMATA) na Chama cha Wachimbaji Wanawake Tanzania (TAWOMA) ambapo  vinajumuisha mitambo mitano ya uchorongaji  yenye thamani ya shilingi bilioni 2.22.  

Vifaa vingine ni pamoja na Lori tatu za kubeba vifusi vya madini (Dump trucks) zenye thamani ya shilingi milioni 544, Lori moja la kubeba mitambo (Lowbed) lenye thamani ya shilingi milioni 274, mtambo mmoja wa kusaga makaa ya mawe (Coal Crusher) wenye thamani ya zhilingi bilioni 1.58.

Pia amekabidhi mtambo mmoja wa kusaga miamba kwa ajili ya kokoto (stone/aggregate crusher) wenye thamani ya shilingi bilioni 1.137, mtambo mmoja wa kufua upepo yaani Air compressor wenye thamani ya Shilingi milioni 424, Lori moja la kubebea maji (water bowser) lenye thamani ya shilingi milioni 210.

Vilevile amekabidhi mitambo miwili ya uzalishaji wa mkaa mbadala (Rafiki Briquettes) wenye uwezo wa kuzalisha tani 20 kwa saa yenye thamani ya shilingi bilioni 2.396, magari mawili (2 hardtop) kwa ajili ya shughuli za uzalishaji madini migodini yenye thamani ya shilingi milioni 317 na Jaw Crusher 10, Metal Detector (20) na Injini ya Dizeli aina ya 24HP moja vyote vikiwa na thamani ya shilingi milioni 72.5.

 

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi