Rais Samia Awasili Ankara Nchini Uturuki kwa Ajili ya Ziara Rasmi
Apr 17, 2024
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwasili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Ankara Esenboga nchini Uturuki kwa ajili ya ziara rasmi tarehe 17 Aprili, 2024.
Na
Ikulu
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na viongozi mbalimbali mara baada ya kuwasili katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Ankara Esenboga nchini Uturuki kwa ajili ya ziara rasmi tarehe 17 Aprili, 2024. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye mazungumzo na Waziri wa Familia na Huduma za Jamii wa Uturuki, Mahinur Ozdemir Goktas mara baada ya kuwasili katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Ankara Esenboga nchini Uturuki kwa ajili ya Ziara Rasmi tarehe 17 Aprili, 2024.