Rais Samia Apokea Miradi Iliyofadhiliwa na Kujengwa na Gaftag
Jul 29, 2021
Na
Jacquiline Mrisho
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, Mhe. Samia Suluhu Hassan, akikata utepe kwa ajili ya kupokea Miradi iliyofadhiliwa na kujengwa na Serikali ya Ujerumani kupitia Jeshi la Nchi hiyo (GAFTAG) kwa Jeshi la Wananchi wa Tanzania JWTZ Lugalo Jijini Dar es salaam Julai 28,2021. kulia ni Balozi wa Ujerumani Nchini Tanzania Bibi. Regine Hess, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe. George Simbachawene, kulia Mkuu wa Majeshi Venance Mabeyo, Waziri wa Afya Mhe. Doroth Gwajima, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje Mhe. Mbarouk Nassor Mbarouk.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, Mhe. Samia Suluhu Hassan,akisoma kibao cha uzinduzi kwa ajili ya kupokea Miradi iliyofadhiliwa na kujengwa na Serikali ya Ujerumani kupitia Jeshi la Nchi hiyo (GAFTAG) kwa Jeshi la Wananchi wa Tanzania JWTZ Lugalo Jijini Dar es salaam leo Julai 28,2021. Kushoto ni Balozi wa Ujerumani Nchini Tanzania Bibi. Regine Hess.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, Mhe. Samia Suluhu Hassan, akipata maelezo kuhusu uchunguzi wa Magonjwa Ambukizi baada ya kupokea Miradi iliyofadhiliwa na kujengwa na Serikali ya Ujerumani kupitia Jeshi la Nchi hiyo (GAFTAG) kwa Jeshi la Wananchi wa Tanzania JWTZ Lugalo Jijini Dar es salaam leo Julai 28,2021. (Picha na Ikulu )