Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Rais Samia Aongoza Marais Afrika Kuwasilisha Ujumbe wa Siku ya Kiswahili
Jul 07, 2022
Na Jacquiline Mrisho

Na Shamimu Nyaki - WUSM

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan ameongoza baadhi Marais wa Afrika kuwasilisha Salamu za Siku ya Kiswahili Duniani Julai 07, 2022.

Mhe.Samia ameishukuru UNESCO kwa kuipa heshima Kiswahili kuwa na Siku ya kuadhimishwa kila Julai 07, kila mwaka.

"Kwa heshima hii tuliyopata kupitia lugha ya Kiswahili, Serikali ya Tanzania itahakikisha nyenzo mbalimbali zinazotakiwa katika kuendeleza lugha hii adhimu ikiwemo kuongeza Bajeti na Wataalamu wa lugha hii zinakuwepo", amesema Mhe. Samia.

Naye Rais wa Jamhuri ya Burundi, Mhe. Evarist Ndaishimiye ameipongeza Tanzania kwa kuadhimisha siku hiyo huku akisisitiza kuwa kiswahili kimeunganisha Waafrika na kimesaidia katika kuleta Uhuru.

Kwa Upande wake Rais wa Msumbiji, Philip Nyusi amesema kuwa Dunia inasherehekea Kiswahili kutokana na kuwa miongoni mwa lugha yenye wazungumzaji wengi ambayo inakadiriwa kuwa na wazungumzaji takriban Milioni 22.

Kilele cha Maadhimisho ya kwanza ya Siku ya Kiswahili Duniani yamezinduliwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi