Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Rais Samia Aleta Nafuu kwa Wawekezaji Kuondoa Tozo za Osha - Katambi
Aug 18, 2023
Rais Samia Aleta Nafuu kwa Wawekezaji Kuondoa Tozo za Osha - Katambi
Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Patrobas Katambi akifafanua jambo kwa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Ustawi na Maendeleo ya Jamii tarehe 18 Agosti, 2023 bungeni jijini Dodoma. Kushoto ni Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Usalama na Afya Mahali pa Kazi (OSHA), Khadija Mwenda.
Na Mwandishi Wetu

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ameendelea kuwathamini wawekezaji kwa kuridhia kupunguzwa na kufutwa baadhi ya tozo zilizokuwa zikitozwa na Wakala wa Usalama na Afya Mahali pa Kazi (OSHA) zenye thamani ya shilingi bilioni 35.

Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Patrobas Katambi ameyasema hayo leo Agosti 18, 2023 jijini Dodoma kwenye kikao na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ustawi na Maendeleo ya Jamii kwa lengo la kuwasilisha taarifa ya utekelezaji wa majukumu na mafanikio ya OSHA.

Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Usalama na Afya Mahali pa Kazi (OSHA), Khadija Mwenda akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa majukumu ya OSHA kwa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Ustawi na Maendeleo ya Jamii, bungeni, tarehe 18 Agosti, 2023, jijini Dodoma.

 

Alisema hatua hiyo ilitokana na ombi la wafanyabiashara kupitia Chama Cha Waajiri Tanzania (ATE) ili kuweka mazingira mazuri kwa wawekezaji nchini.

Katambi alisema masuala ya usalama na afya mahali pa kazi yataendelea kupewa uzito na serikali ili kuhakikisha nguvu kazi iliyopo inakuwa salama.

Naye, Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ustawi na Maendeleo ya Jamii, Mhe. Fatuma Toufiq alipongeza serikali kwa kuendelea kufanyia kazi maoni ya kamati ya kuimarisha masuala ya usalama mahali pa kazi kwa kuipatia OSHA vitendea kazi ili itekeleze majuku yake kwa ufanisi zaidi.

Baadhi ya Wajumbe wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Ustawi na Maendeleo ya Jamii, wakifuatilia kwa makini maelezo ya Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Usalama na Afya Mahali pa Kazi (OSHA), Khadija Mwenda (hayupo pichani) wakati akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa majukumu ya OSHA, bungeni, tarehe 18 Agosti, 2023, jijini Dodoma.

 

Kwa upande wake, Mtendaji Mkuu wa OSHA, Khadija Mwenda, alisema tozo ya upimaji umeme katika vituo vya mafuta hasa maeneo ya vijijini imepunguzwa kutoka shilingi 650,000 hadi shilingi 150,000 ili kuvutia wawekezaji na kuondokana na mafuta kuuzwa kwenye chupa.

Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ustawi na Mendeleo ya Jamii Mhe. Fatuma Toufiq (kushoto) akizungumza jambo mara baada ya kupokea taarifa ya utekelezaji wa majukumu ya OSHA, leo tarehe 18 Agosti, 2023 Bungeni jijini Dodoma. Kulia ni Katibu wa kamati hiyo Bi. Aziza Kheir. 

 

Alisema kumekuwa na matokeo chanya ambapo OSHA imevifikia vituo 2,708 ikilinganishwa na kabla ya kupunguzwa tozo vilifikiwa vituo 1,153.

Kadhalika, alisema kutokana na Tanzania kutekeleza kwa kiwango kikubwa masuala ya usalama na afya mahali pa kazi, imekuwa mfano kwa mataifa mengine kuja kujifunza.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi