Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan amefanya ziara ya Kihistoria Tanga huku akipokewa na watu maelefu kwa maelefu.
Huku vifijo na nderemo vikitawala kila alikopita.
Kiongozi shupavu wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan amefurahishwa na kuridhishwa na utekelezaji wa miradi ya maendeleo.
Mapokezi hayo yanaakisi jinsi wananchi wanavyokubali kazi kubwa inayofanywa na Kiongozi shupavu wa Tanzania, Dkt Samia Suluhu Hassan ambaye amefurahishwa na kuridhishwa na utekelezaji wa miradi ya maendeleo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan amesema ameridhishwa na matumizi ya fedha za ujenzi wa miradi ya maendeleo mkoani Tanga na kuwapongeza wasimamizi wa fedha hizo.
"Nimekuja kuwasalimia na kuangalia matumizi ya fedha zinazoletwa kuwasaidia wananchi kama kweli zimeondoa shida za wananchi, sitaki nilaumu kwa kiasi kikubwa jana na leo nimeona fedha zimetumika vizuri", amesema Rais Samia.
Amesema madhumuni ya miradi hiyo ni kusogeza huduma kwa wananchi na kuimarisha utawala bora.
Katika ziara hiyo baadhi ya viongozi walimwambia Rais kuwa wanakabiliwa na changamoto ya wanyamapori ambapo amesema anaitambua changamoto hiyo na Serikali imekuwa ikichukua hatua mbalimbali kwa ajili ya kuwalinda wananchi ikiwepo kuongeza askari wa wanyamapori na kubuni mbinu mbalimbali za kufukuza wanyama na matumizi ya ndege nyuki.
Amemwagiza Waziri wa Maliasili na Utalii, Balozi Pindi Chana aangalie uwezekano wa kufanya mapitio ya kanuni za fidia kwa wanaoingiliwa kwenye mashamba yao.