Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Rais Mwinyi Awasili Chato
Jan 14, 2021
Na Msemaji Mkuu

Na Mwandishi Maalum - CHATO

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi amewasili mjini Chato leo kwa mazungumzo na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli.

Kiongozi huyo wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar amepokelewa na viongozi mbalimbali akiwemo Waziri wa Nishati na Mbunge wa Jimbo la Chato, Mhe. Dkt. Medard Kalemani.

Rais Dkt. Mwinyi anatarajiwa kuzungumza na Mwenyeji wake hapo baadae leo.

Hii ni ziara ya kwanza ya Rais Mwinyi tangu alipoapishwa kuwa Rais wa Zanzibar mnamo Novemba 2, 2020.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi