Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan Azindua na Kugawa Vitendea Kazi Mbalimbali kwa Maafisa Ugani Kilimo Nchini
Apr 05, 2022
Na
Jacquiline Mrisho
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akiangalia miche ya matunda ya miembe pamoja na michungwa katika mabanda ya maonesho ya bidhaa za kilimo nje ya ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete Jijini Dodoma leo tarehe 04 Aprili, 2022.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akizungumza na Viongozi mbalimbali kabla ya kuzindua na kugawa vitendea kazi kwa Maafisa Ugani wa Kilimo katika hafla iliyofanyika katika ukumbi wa Jakaya Kikwete Jijini Dodoma leo tarehe 04 Aprili, 2022.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akiangalia aina mbalimbali ya zao la mpunga ambao umekobolewa katika viwango mbalimbali kwa ajili ya matumizi ya binadamu na utengenezaji wa nafaka kwa ajili ya mifungo katika maonesho yaliyofanyika nje ya ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete Jijini Dodoma leo tarehe 04 Aprili, 2022.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akiangalia mchele uliowekwa kwenye kifungashio kwa ajili ya kupelekwa sokoni katika maonesho yaliyofanyika nje ya ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete Jijini Dodoma leo tarehe 04 Aprili, 2022. Kushoto ni Waziri wa Kilimo Hussein Bashe
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akimsikiliza Mwenyekiti wa Baraza la Kilimo la Taifa, Jacqueline Mkindi kuhusu zao jipya la kilimo pamoja na mazao mbalimbali ya Biashara katika maonesho yaliyofanyika nje ya ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete Jijini Dodoma leo tarehe 04 Aprili, 2022.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akiwa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati wakimsikiliza Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe kuhusu zao la parachichi ambalo limekuwa likiwaletea tija wakulima nchini hususan katika Mikoa ya Njombe, Mbeya, Arusha na Kilimanjaro.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akimsikiliza Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe mara baada ya ukaguzi wa mabanda mbalimbali ya wakulima pamoja na Wafanyabiashara leo tarehe 04 Aprili, 2022 Jijini Dodoma.
Wananchi pamoja na wadau mbalimbali wa Kilimo wakiwa katika ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete Jijini Dodoma kwa ajili ya kushuhudia uzinduzi na ugawaji wa vitendea kazi kwa Maafisa Ugani wa Kilimo nchini uliofanywa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan leo tarehe 04, Aprili, 2022.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Samia Suluhu akiwasha Pikipiki mara baada ya kuzindua ugawaji wa pikipiki hizo 7000 kwa ajili ya Maafisa Ugani nchini.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Samia Suluhu akiwa na Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa, Waziri wa Kilimo, Mhe. Hussein Bashe, Naibu Waziri wa Kilimo, Antony Mavunde pamoja na Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Ndugu Daniel Chongolo wakati akikata utepe kuashiria uzinduzi wa ugawaji wa pikipiki 7000 kwa ajili ya Maafisa Ugani Kilimo wa nchi nzima katika hafla iliyofanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete Jijini Dodoma leo tarehe 04 Aprili, 2022