Rais Mhe. Samia Awapongeza Serengeti Girls Ikulu Jijini Dar es Salaam
Jul 05, 2022
Na
Jacquiline Mrisho
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimpa zawadi Nahodha wa Timu ya Taifa ya Wanawake wenye umri chini ya miaka 17 (Serengeti Gils) Noela Luhala kwa niaba ya Wachezaji wenzake kwenye hafla ya kuwapongeza iliyofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 05 Julai, 2022.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa na Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mohamed Mchengerwa, Katibu wa Wizara hiyo, Dkt. Hassan Abbasi, Rais wa Shirikisho la Mpira wa miguu nchini (TFF), Bw. Wallace Karia katika picha ya Pamoja na Timu ya Taifa ya Wanawake wenye umri chini ya miaka 17 (Serengeti Gils) kabla ya hafla ya kuwapongeza iliyofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam.