Rais Mhe. Samia Apokea Machapisho ya Sensa ya Watu na Makazi ya Mwaka 2022
Aug 17, 2023
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akipokea Machapisho ya Sensa ya Watu na Makazi ya Mwaka 2022 kutoka kwa Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa wakati wa Kikao kilichofanyika Ikulu mkoani Dodoma tarehe 17 Agosti, 2023.
Na
Ikulu
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Viongozi mbalimbali mara baada ya kupokea Machapisho ya Sensa ya Watu na Makazi ya Mwaka 2022, Ikulu mkoani Dodomatarehe 17 Agosti, 2023.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya kumbukumbu na Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa, Katibu Mkuu Kiongozi, Mhe. Balozi Dkt. Moses Kusiluka, Kamisaa wa Sensa, Tanzania Bara Spika Mstaafu, Mhe. Anne Makinda, Kamisaa wa Sensa, Zanzibar Mhe. Balozi Mohammed Hamza pamoja na Watakwimu mara baada ya kupokea Machapisho ya Sensa ya Watu na Makazi ya Mwaka 2022, Ikulu mkoani Dodoma tarehe 17 Agosti, 2023.
Kamisaa wa Sensa ya Watu na Makazi Tanzania Bara Spika Mstaafu, Mhe. Anne Makinda akizungumza na Viongozi mbalimbali wakati wa Kikao kilichofanyika Ikulu mkoani Dodoma tarehe 17 Agosti, 2023.