Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

RAIS MAGUFULI: VIONGOZI WA AFRIKA TUBADILI MTAZAMO KUHUSU DHANA YA USHIRIKIANO NA MATAIFA TAJIRI
Nov 08, 2019
Na Msemaji Mkuu

[caption id="attachment_48713" align="aligncenter" width="750"] Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli akiwa kwenye Mkutano wa Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Nchi za Afrika na Nordic uliofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa Julius Nyerere, Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba Kabudi na Kushoto ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, Mhe. George Simbachawene na Waziri wa Mamba ya Nje kutoka Norway, Ine Eriksen Soreide.[/caption]

 Na Mwandishi Wetu

RAIS Dkt. John Magufuli amewataka Viongozi wa Bara la Afrika kubadili fikra na mtazamo wa kutegemea misaada na utegemezi wa kiuchumi kutoka nchi tajiri na badala yake kutumia diplomasia ya uchumi kuwa msingi wa ushirikiano katika kuleta maendeleo ya haraka kwa wananchi wake.

Akizungumza katika ufunguzi wa Mkutano  wa 18 wa Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Nchi za NORDIC na Bara la Afrika ulioufunguliwa leo Ijumaa (Novemba 8, 2019) Jijini Dar es Salaam, Rais Magufuli alisema uhuru wa kisiasa uliozipata Nchi za Bara la Afrika hautakuwa maana iwapo Nchi zake zitaendelea klwa wategemezi wa misaada kutoka Nchi tajiri.

[caption id="attachment_48714" align="aligncenter" width="750"] Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia kwenye Mkutano wa Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Nchi za Afrika na Nordic uliofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa Julius Nyerere Dar es Salaam Loe novemba 8, 2019.[/caption]

Rais Magufuli alisema kuwa Bara la Afrika lina mambo mengi mazuri yanayopaswa kuwekewa kipaumbele katika kujikwamua kiuchumi kupitia ushirikiano wake na Nchi za NORDIC ikiwemo fursa za biashara na uwekezaji, hivyo kuliweka katika ajenda muhimu inayopaswa kuwekeza msisitizo.

‘Ushirkiano wetu na Nchi za NORDIC kwa miaka mingi umekuwa ni utegemezi wa kiuchumi, Viongozi wa Afrika tunapaswa kutambua kuwa mustakabali wa mataifa yetu upo mikononi mwetu, ni lazima tuondokane na aina hii ya ushirikiano’’ alisema Rais Magufuli.

Aidha Rais Magufuli alisema Bara la Afrika lina utajiri mkubwa wa raslimali na vivutio mbalimbali vya biashara na uwekezaji ukilinganisha na Nchi za NORDIC, lakini hata hivyo Mataifa hayo ya NORDIC yamekuwa yakipiga hatua kubwa za maendeleo ya kiuchumi ikilinganisha na Nchi za Bara la Afrika.

[caption id="attachment_48715" align="aligncenter" width="750"] Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia kwenye Mkutano wa Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Nchi za Afrika na Nordic uliofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa Julius Nyerere, kutoka kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba Kabudi, Waziri wa Mamba ya Nje kutoka Norway, Ine Eriksen Soreide na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, Mhe. George Simbachawene.[/caption]

Akitoa mfano Rais Magufuli alisema katika Nchi tano za NORDIC zenye ukubwa wa kilometa za mraba Milioni 3.5 na mwaka 2018 zilikuwa na  Pato la Taifa la Dola Trilioni 1.7 kwa mwaka huku idadi ya wananchi wake ikiwa ni Milioni 27 wakati Bara la Afrika lenye watu Bilioni 1.2 mwaka 2018 lilikuwa na Pato la taifa lenye thamani ya Dola trilioni 2.334, na kuongeza kuwa Nchi za Bara la Afrika lipo jambo linalopaswa kujifunza.

Aidha Rais Magufuli alisema ni wajibu wa Viongozi wa Bara la Afrika kuweka nguvu ya pamoja katika kusimamia rasilimali na maliasili ilizonazo kwa ajili ya kuleta ustawi wa maendeleo katika sekta mbalimbali za kiuchumi ikiwemo kilimo, madini, misitu, mafuta, gesi, nishati na mifugo

[caption id="attachment_48716" align="aligncenter" width="750"] Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba Kabudi, akitoa hotuba fupi ya kumkaribisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli kuhutubia Mkutano wa Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Nchi za Afrika na Nordic uliofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa Julius Nyerere, Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Loe novemba 8, 2019.[/caption]

‘Asilimia 30 ya ardhi bora ya kilimo duniani ipo Afrika, na kwa mujibu wa takwimu zilizopo Kati ya Nchi 10 bora zinazoongoza kwa kasi ya ukuaji uchumi duniani, Nchi 5 zinatoka Bara la Afrika, hii ni fursa ambayo haina budi kuitumia Afrika katika kuleta maendeleo kwa ustawi wa wananchi’’ alisema Rais Magufuli.

Akifafanua zaidi Rais Magufuli alisema Tanzania kwa upande wake imepiga hatua kubwa za maendeleo katika Nchi za Bara la Afrika kwa kuwa imeimarisha sekta mbalimbali za kijamii na kiuchumi kwa wananchi wake ikiwemo ujenzi wa miundombinu ya usafiri na kuweka mazingira  bora ya uwekezaji.

[caption id="attachment_48717" align="aligncenter" width="750"] Waziri wa Mamba ya Nje kutoka Norway, Ine Eriksen Soreide akizungumza katika Mkutano wa Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Nchi za Afrika na Nordic uliofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa Julius Nyerere Dar es Salaam Loe novemba 8, 2019.[/caption]

Aidha aliwataka Viongozi wa NORDIC kutumia fursa zilizopo katika Bara la Afrika kwa ajili ya kusaidia ujenzi wa viwanda vya malighafi, kwa kuwa bidhaa nyingi za Afrika zimekuwa zikisafirishwa kwenda kuuzwa nje ya Nchi, hivyo wawekezaji hawana budi kuitumia fursa hiyo kwa ajili ya kuleta maendeleo ya Bara la Afrika.

Kwa upande wake, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wa Tanzania, Prof. Palamagamba Kabudi alisema kwa miaka mingi sasa Nchi za NORDIC zimekuwa rafiki wa kweli kwa Nchi za Bara Afrika ikiwemo Tanzania ambapo tangu uhuru wa Tanzania Nchi hizo zimekuwa zikisaidia ujenzi wa miradi mbali ya maendeleo nchini.

[caption id="attachment_48719" align="aligncenter" width="750"] Wajumbe wa Mkutano wa Mawaziri wa Nchi za Afrika na Nordic wakifuatilia hotuba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli, katika Mkutano wa Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Nchi za Afrika na Nordic uliofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa Julius Nyerere Dar es Salaam Loe novemba 8, 2019.[/caption]

Kwa mujibu wa Prof. Kabudi alisema katika Mkutano huo, Mawaziri wa Nchi za NORDIC na wale wa Bara la Afrika watapata fursa ya kujadiliana masuala mbalimbali ikiwemo diplomasia ya uchumi na masuala ya ulinzi na usalama na kuweka mkakati wa pamoja utakaowezesha nchi hizo kufikia malengo waliyojiwekea.

[caption id="attachment_48720" align="aligncenter" width="750"] Washiriki wa Mkutano wa Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Nchi za Afrika na Nordic, kutoka nchi za Nordic wakifuatilia Mkutano huo uliofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa Julius Nyerere Dar es Salaam Loe novemba 8, 2019.[/caption]

‘Suala la Mpango wa Maendeleo Endelevu wa mwaka 2030 pia ni moja ya maeneo yatakayojadiliwa na Mawaziri wa Nchi hizi, tutaliangalia kwa undani zaidi suala la mabadiliko ya tabia nchi katika namna bora ya kukabiliana na changamoto zake katika Mataifa yetu ya Bara la Afrika’’ alisema Prof. Kabudi.

[caption id="attachment_48721" align="aligncenter" width="750"] Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli, akiwa katika picha ya pamoja na Mawaziri wa Nchi za Afrika na Nordic Mara baada ya kufungua Mkutano huo uliofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa Julius Nyerere Dar es Salaam Loe novemba 8, 2019.[/caption]

Naye Waziri wa Mambo ya Nje wa Norway, Ine Eriksen Soreide alisema Nchi za NORDIC zitaendeleakushirkiana na Mataifa ya Bara la Afrika katika kuleta maendeleo ya wananchi pamoja na mipango ya pamoja ya kukabiliana na matishio mbalimbali ya binadamu ikiwemo ugaidi na magonjwa ya milipuko.

Nchi za NORDIC zitaundwa na Nchi tano za Sweden, Norway, Finland, Iceland na Denmark pamoja ikiwa na ushirikiano wa Nchi 29 za Bara la Afrika.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi