Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Rais Magufuli Kuongoza Mapokezi ya Ndege Kesho
Jul 07, 2018
Na Msemaji Mkuu

Ikulu, Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli kesho Jumapili tarehe 08 Julai, 2018 atawaongoza Watanzania katika mapokezi ya ndege mpya aina ya Boeing 787-8 Dreamliner iliyonunuliwa na Serikali ya Tanzania.

Ndege hiyo inatarajiwa kutua katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam majira ya saa 8:00 Mchana, ikitokea Seattle nchini Marekani.

Hii ni ndege ya 4 kuwasili nchini kati ya ndege 7 zilizonunuliwa na Serikali ya Tanzania kwa ajili ya kuliwezesha Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) kuimarisha huduma zake.

Wananchi mnakaribishwa katika tukio hilo ama kufuatilia matangazo ya mapokezi kupitia vyombo vya habari vya redio, televisheni, mitandao ya kijamii na tovuti rasmi ya Ikulu ambayo ni www.ikulu.go.tz

Gerson Msigwa

Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU

Dar es Salaam

07 Julai, 2018

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi