Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Rais Magufuli Azindua Shule, Chuo cha VETA Kagera
Jan 18, 2021
Na Msemaji Mkuu

Na Redempta Ndubuja

Rais   wa    Jamuhuri  ya Muungano  wa  Tanzania, Dkt. John Pombe  Magufuli   amezindua  ujenzi  wa Chuo  cha  Ufundi  Stadi  (VETA) kilichopo   mkoani  Kagera na kuzindua  Shule   ya  Sekondari  ya  Ihungo  iliyobomolewa na tetemeko mnamo 2016.

Akizungumza baada ya uzinduzi huo, Rais  Magufuli amesema Chuo cha VETA kimejengwa kwa shilingi bilioni 22 huku shule ya sekondari ya Ihungo ikijengwa kwa shilingi bilioni 10.9.

“Kuna kero ya kutokamilika kwa jengo la mama na mtoto katika Zahanati ya Buhembe ambapo shilingi milioni 229 zilitolewa na UNDP kwa ajili yaujenzi wa jengo hilo lakini jengo halijakamilika na fedha zimeisha, Mkurugenzi jipange vizuri ili jengo likamilike” amesema Mheshimiwa Rais.

Naye, Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Joyce Ndalichako amesema Chuo cha VETA kitachukua wanafunzi 800 wa kozi ndefu na 1,000 wa kozi fupi huku shule iliyojengwa ikiwa na uwezo wa kuchukua wanafunzi 1,150.

“Pamoja na mradi huu, Serikali inaendelea na ukarabati wa shule kongwe 89 ambapo shule 86 zimeshakarabatiwa na nyingine zipo kwenye za mwisho za ukarabati” amesema Mheshimiwa Waziri.

Kwa upande wake,  Mkuu wa Mkoa  wa Kagera,  Brigedia  Jenerali Marco  Kaguti amesifu maendeleo yaliyopatikana kwenye sekta ya elimu katika muhula wa kwanza wa utumishi wa Rais Magufuli.

“Ufaulu  nao  umeongezeka,   kwa sasa  ufaulu kwenye Mkoa  wa  Kagera  ni  asilimia  88.8 kwa shule za msingi na ufaulu wa shule za sekondari   umefikia asilimia 90” amesema Mheshimiwa Kaguti.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi