Jonas Kamaleki - MAELEZO
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amewataka viongozi walioapishwa kutekeleza majukumu yao kwa kufuata sheria katika kuwatumikia wananchi.
Rais Magufuli amayasema hayo leo Ikulu jijini Dar es Salaam wakati akiwaapisha, Makatibu Wakuu, Manaibu Katibu Wakuu na Wakuu wa Mikoa aliowateua jana.
Amewataka viongozi hao kuwatumikia wananchi kwa kuongeza ubunifu ili kuinua uchumi na kutatua kero zao hasa za wananchi wanyonge.
“Nataka mkawe sauti yao, mumtangulize Mungu katika kuwatumikia watu wake,”aliwaasa Rais Magufuli.
[caption id="attachment_21119" align="aligncenter" width="750"]Rais Magufuli amewataka viongozi hao kufanya kazi kwa bidii ili kujenga Tanzania mpya yenye uchumi mzuri na kuifanya nchi kuwa ya kuvutia.
Aidha, Rais Magufuli amewaambia wakuu wa mikoa waangalie nini kinaweza kufanyika katika maeneo yao ili kuinua uchumi wa wananchi waishio katika mikoa hiyo.
Akizungumza kuhusu Makatibu na Manaibu wao, Rais Magufuli amewataka watatue kero na changamoto zilizopo kwenye wizara zao.
“Nyote niliowateua msijifanye wageni katika wizara au mikoa yenu, leo nikitaka kujua habari za korosho Ruvuma nakupigia simu na nataka nizipate hapo hapo,” alisema Rais Magufuli.
Kwa upande wake, Makamu wa Rais, Mhe. Samia Suluhu Hassan amesema kuwa viongozi hao wameapa kuwatumikia wananchi bila upendeleo wala ubaguzi na kuwataka wafanye hivyo hivyo maana kiapo kinaduma.
“Wakuu wa mikoa tungependa kuona utumishi uliotukuka kutoka kwenu,” alisema Mhe. Samia Suluhu.
Amewataka Wakuu wa mikoa kuwa makini katika kufanya maamuzi na kuwaambia wafikiri mara tatu kabla ya kufanya maamuzi kwa kuangalia athari za kiuchumi, kisiasa na kijamii.
[caption id="attachment_21121" align="aligncenter" width="750"]Naye Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Job Ndugai ameahidi kutoa ushirikiano kwa viongozi walioapishwa ili kuijenga Tanzania.
Akitoa salamu zake katika hafla hiyo, Jaji Mkuu wa Tanzania, Prof. Ibrahim Juma amesema viongozi walioapishwa wazingatie sheria katiak utekelezaji wa majukumu yao.
[caption id="attachment_21122" align="aligncenter" width="750"]Amewataka wakuu wa mikoa kufanya kazi zao kwa uadilifu kwani wao ndio wenyeviti wa kamati za maadili za mikoa, hivyo hawapaswi kulalamika kuhusu uadilifu.
Rais Magufuli amewaapisha Makatibu Wakuu 4, Manaibu 7 na Wakuu wa Mikoa 6 ambapo Rais amembadilishia kituo cha kazi Mhe. Christina Mdeme kuwa Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma badala ya Dodoma na kumhamisha aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Dkt. Binilith Mahenge kwenda Dodoma.
[caption id="attachment_21123" align="aligncenter" width="768"]