Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Rais Magufuli Avunja Wakala wa Uendelezaji Mji Kigamboni
Sep 13, 2017
Na Msemaji Mkuu

Na: Mwandishi Wetu

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mheshimiwa William Lukuvi ametangaza rasmi kwamba Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa John Pombe Magufuli ameivunja rasmi Wakala wa Uendelezaji Mji wa Kigamboni (KDA) kuanzia leo.

Aidha Mheshimiwa Rais ameelekeza kwamba shughuli zote zilizokuwa zinafanywa na KDA sasa zifanywe na Manispaa ya kigamboni kwa mujibu wa sheria.

Kutokana na kuvunjwa kwa KDA, kuanzia sasa Manispaa ya Kigamboni itahusika kupanga na kusimamia ardhi yake kama manispaa nyingine zinavyofanya na Wizara ya Ardhi itaendelea kusimamia masuala yote yahusuyo ardhi kwa ujumla wake kama inavyofanya katika manispaa zote nchini.

Waziri wa Ardhi pia akatangaza kwamba kuanzia sasa wakazi wa mji wa Kigamboni wasizuiliwe kupewa hati zao za umiliki wa ardhi na wasizuiliwe kupewa vibali vya ujenzi.

Mheshimiwa Lukuvi pia amefuta mashamba mawili yalioko wilayani kigamboni jijini Dar es salaam na kurudisha mashamba hayo kwa serikali ya wilaya ya kigamboni.

Ufutaji hu ni baada ya wamiliki hao kushindwa kuyaendeleza na kuwanyima fulsa wananchi kufanya shughili zingine na kuinyima wilaya kufanya shuguli za viwanda na uwekezaji mwingine kutokana na kuhodhi kwa maeneo hayo.

Nae mbuge wa wa Kigamboni Dr. Faustine Ndugulile ametoa shukrani zake kwa Rais kwani Muingiliano wa  majukumu wa mamlaka hizo ulikuwa ukiwabana wananchi hivyo kuwasababishia  kushindwa kufanya shuguli za maendeleo.

Nao baadhi ya wananchi wa Kigamboni wamefurahishwa sana na maamuzi ya Rais kuhusu kuvunjwa kwa Wakala wa Uendelezaji wa Mji wa Kigamboni (KDA) kwani ulikuwa unawapa wakati mgumu katika kuendeleza maeneo yao na kuleta urasimu.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi