Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Rais Magufuli Atoa Zawadi ya Idd El Fitri Yenye Thamani ya Mil. 10.9
Jun 24, 2017
Na Msemaji Mkuu

[caption id="attachment_4324" align="aligncenter" width="800"] Kamishna Msaidizi katika Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Simon Panga, akizungumza kabla ya kukabidhi zawadi ya Idd El Fitri kwa niaba ya Rais Dk. John Magufuli kwaVituo vya Yatima na Makundi Maalumu katika Maabusu ya Watoto Dar es Salaam, leo.[/caption]

Na. Lilian Lundo

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli ametoa zawadi ya Idd El Fitri zenye thamani ya shilingi 10,922,000 kwa vituo 9 vya Mkoa wa Dar es Salaam, vituo 2 vya Zanzibar na vituo 13 kutoka mikoa ya Tanzania Bara.

Zawadi hizo zimekabidhiwa leo, Jijini Dar es Salaam na Kamishina Msaidizi wa Ustawi wa Jamii, Idara ya ustawi wa Jamii, Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee, na Watoto, Simon B. Panga kwa niaba ya Mhe. Rais, Dkt. John Magufuli

[caption id="attachment_4325" align="aligncenter" width="534"] Kamishna Msaidizi katika Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Simon Panga, akikabidi zawadi kwa Ofisa Ustawi wa Jamii Mfawidhi wa Makao ya Taifa ya Yatima Kurasini, Dar es Salaam, Beatrice Mgumiro.[/caption]

Panga amezitaja zawadi zilizotolewa kuwa ni mchele, mbuzi na mafuta ya kupikia ambazo zitawezesha makundi hayo kufurahi na kusherehekea sikukuu kama ilivyo kwa watu wengi.

“Mhe. Rais kwa upendo wake wa dhati kabisa ameona umuhimu wa kushiriki pamoja na watu walio katika makundi maalum wakiwemo watoto walio katika mazingira hatarishi na wazee  wenye ulemavu wasiojiweza, wanaohudumiwa  katika makazi katika kusherehekea sikukuu ya Idd El Fitri mwaka 2017,” amesema Panga.

Panga amevitaja vituo vilivyonufaika na zawadi za Mhe. Rais kwa Mkoa wa Dar es Salaam ni Makao ya Taifa ya Watoto Yatima Kurasini – Temeke, Makao ya Watoto IBN Kathry- Ilala, Makao ya Watoto Yatima Msimbazi, Makao ya Watoto Yatima Chakuwama, Makao ya Watoto Yatima Group Trust Fund – Temeke, Makao ya Watoto Yatima Dar Al Arqum (International Islamic Relief Organization), Mahabusu ya Watoto Dar es Salaam – Upanga, Makazi ya Wazee na Wasojiweza Nunge – Kigamboni na Shule ya Ufundi ya Watoto Wenye Ulemavu Yombo.

[caption id="attachment_4330" align="aligncenter" width="800"] . Kamishna Msaidizi katika Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Simon Panga, akikabidhi zawadi wa Sister Stella Selugenge wa Makao ya Yatima Msimbazi, Dar es Salaam.[/caption]

Aidha, amevitaja vituo vilivyonufaika kwa upande wa mikoa ya Tanzania Bara kuwa ni Makao ya Watoto Tosamaganga – Iringa, Makao ya Watoto Yatima Malaika Kids Home, Mkuranga – Pwani, Makao ya Watoto  Yatima Karibu Nyumbani, Kibaha – Pwani, Makao ya Watoto Yatima Miyuji Cheshire – Dodoma, Shule ya Maadilisho Irambo – Mbeya na Mahabusu ya Watoto – Mbeya.

Vituo vingine ni Mahabusu ya Watoto – Arusha, Makao ya Wazee na Wasiojiweza Kolandoto – Sinyanga, Makazi ya Wazee na Wasiojiweza Ngehe – Ruvuma, Makazi ya Wazee na Wasiojiweza Kiilima – Bukoba, Kagera, Makazi ya Wazee na Wasiojiweza Magugu – Manyara, Makazi ya Wazee na Wasiojiweza Ipuli – Tabora, Makazi ya Wazee na Wasiojiweza Bukumbi – Mwanza.

Kwa upande wa Zanzibar, vituo vilivyonufaika ni Kituo cha Watoto Yatima Mabaoni – Chakechake – Pemba na Makazi ya Wazee na Wasiojiweza Sebleni – Unguja.

Utoaji wa zawadi hizi ni utaratibu wa Waheshimiwa Marais tangu awamu nne zilizopita ambapo wamekuuwa wakiwapatia makundi hayo maalum zawadi za vyakula katika sikukuu mbalimbali

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi