Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Rais Magufuli Ataka Wawekezaji Makini katika Umeme
Apr 03, 2018
Na Msemaji Mkuu

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizindua mradi wa kuzalisha umeme MW 240 wa Kinyerezi ll eneo la Kinyerezi jijini Dar es salaam leo Aprili 3, 2018

Na. Immaculate Makilika- MAELEZO

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John  Pombe Magufuli  amewakaribisha wawekezaji katika  sekta ya umeme  ili kuongeza  ufanisi wa uzalishaji wa nishati hiyo nchini.

Amesema hayo alipokuwa akizindua mtambo wa kisasa wa kufua umeme asilia ulipo Kinyerezi jijini Dar es salaam. “Yeyote mwenye nia ya kuwekeza tunamruhusu aje, anayekuja kwa nia ya dhati ya kushirikiana sio kutukomoa, tunamruhusu” alisisitiza Rais Magufuli.

Aidha, Rais Magufuli alisema kuwa mtambo huo wa Kinyerezi II wa kuzalisha umeme ni katika ukanda huu wa Afrika Mashariki, ambapo  umeme  unasaidia katika unaendelezaji wa shughuli mbalimbali za kimaendeleo na uchumi wa viwanda .

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipata maelezo toka kwa Waziri wa Nishati Dkt. Menard kalemani,  kabla ya kuzindua mradi wa kuzalisha umeme MW 240 wa Kinyerezi ll eneo la Kinyerezi jijini Dar es salaam leo Aprili 3, 2018

Rais Magufuli pia ameziomba Taasisi za umma  na binafsi za ndani na nje ya nchi kuchangamkia fursa ya kusambaza umeme asilia na wa jua ili kupunguza athari za matumizi ya mkaa nchini.

“Mahitaji ya umeme ni megawati 1400, na uzalishaji ni megawati 1500 ambapo zinahitajika jitihada za kufua na kusafirisha umeme.  36.6% tu ya wananchi wa ndio wenye umeme, na 60% bado hawana umeme, hata hivyo muanze kufikiria kupunguza bei ya umeme ili wananchi waweze kutumia nishati hiyo” alisema Rais Magufuli

Mradi huo wa Kinyerezi II ulioanza kutekelezwa Machi 1 mwaka jana, unaongeza megawati 240 katika gridi ya Taifa, ambapo hadi kukamilika kwake utagharimu shilingi bilioni 758, ambapo Serikali imeshalipa asilimia 15 ya fedha zote za mradi.

Aidha, akizungumza katika uzinduzi huo Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani alisema kuwa mitambo yote 6 ya mradi huo tayari imeanza kuingiza umeme katika gridi ya Taifa na taratibu nyingine zinaendelea  ikiwa mradi huo umekamilika siku  45 kabla ya wakati.

Baadhi ya wananchi wa Dar es Salaam wakiwa wakisikiliza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. John Pombe Magufuli wakati wa uzinduzi wa mitambo ya kufua umeme ya Kinyerezi II wenye uwezo wa 240MW. Sherehe za uzinduzi huo zilifanyika leo eneo la Kinyerezi, Jijini Dar es Salaam.

Waziri Kalemani alisema kuwa katika miaka 4 ijayo Kinyerezi itazalisha megawati 1692. Pia alitaja miradi mingine kuwa ni Mtwara utakaozalisha umeme wa gesi megawati 300  na kugharimu dola za kimarekani 365, mradi wa  mkubwa wa kuzalisha umeme  Sumbawanga – Kigoma- Nyakazi  utakaogharimu  dola za kimarekani 664 , ambapo mradi huo utasaidia kumaliza tatizo la umeme katika mikoa ya kusini. Pamoja na mradi wa Singida – Namanga utakaozalisha megawati 400.

|Naye, Mkurugenzi wa  Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO)  Tito Mwinuka, alisema kuwa ili kukabiliana na tatizo la nishati hiyo nchini, imeandaliwa miradi 4 kwa ajili ya kufua umeme wa kutumia gesi asilia  ambapo mradi wa upanuzi wa Kinyerezi I unaozalisha megawati 185 na kukamilika mwa ka 2019  na Kinyerezi II megawati 240 utakaokamilika hivi karibuni.

Miradi mingine ni Kinyerezi III utakazozalisha megawati 600 na Kinyerezi IV utakaozalisha megawati 450 kwa kutumia gesi asilia kutoka Nazi Bay mkoani Mtwara.

Vilevile, Mwakilishi wa Balozi wa Japan nchini Hiroyuki Kubota alisema kuwa  serikali yake itaendelea kushirikiana na Tanzania katika kusaidia kutekeleza sera ya viwanda na kuendeleza maendeleo ya jamii, ikiwa nai pamoja na kukuza uchumi.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi