Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Rais  Magufuli   Apongezwa  Dhana ya Uchumi wa Viwanda
Feb 06, 2019
Na Msemaji Mkuu

[caption id="attachment_40160" align="aligncenter" width="900"] Muonekano Kiwanda cha kuzalisha Sayona Drinks Limited kilichopo Chalinze mkoani Pwani, kujengwa kwa kiwanda hicho ni matokeo ya dhana ya ujenzi wa viwanda inayosisitizwa na Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais, Dkt John Pombe Magufuli. Kiwanda hicho kimejengwa kwa gharama ya dola za kimarekani milioni 53 na kutoa ajira kwa wananchi zaidi ya 450, maji ya matunda yanayozalishwa na kiwanda hicho yanatokana na maembe, mapera na machungwa. Aidha, kiwanda hicho kimekuwa chachu kwa wakulima kuongeza uzalishaji wa matunda hapa nchini.[/caption] [caption id="attachment_40155" align="aligncenter" width="900"] Sehemu ya mitambo ya Kiwanda cha kuzalisha juisi cha Sayona kilichopo Chalinze mkoani Pwani. Kiwanda hicho kimetoa ajira kwa mamia ya wananchi na kuchangia katika kukuza uchumi.[/caption] [caption id="attachment_40150" align="aligncenter" width="900"] Sehemu ya mitambo ya Kiwanda cha kuzalisha juisi cha Sayona kilichopo Chalinze mkoani Pwani. Kiwanda hicho kimetoa ajira kwa mamia ya wananchi na kuchangia katika kukuza uchumi.[/caption]

Na: LilianLundo – MAELEZO

Mkurugenzi Mkuu wa Sayona Drinks Limited na Mwenyekiti wa Wamiliki wa Viwanda nchini, Subhash Patel amempongeza Mhe. Rais Magufuli juu ya dhana ya uchumi wa viwanda nchini ambao umeonesha mafanikio makubwa katika kipindi cha miaka mitatu tangu aingie madarakani.

Patel ameyasema hayo wakati wa mahojiano maalum  katika kiwanda chake cha Sayona  kilichopo Chalinze, mkoani  Pwani.

“Viwanda vingi tulivyovianzisha vimetokana  na kauli ya Mhe. Rais ya kujenga uchumi wa viwanda. Rais Magufuli ameitoa dhana hii kutoka rohoni kwake, tunampongeza na tunaona namna inavyofanikiwa,” amesema Patel.

Amesema, katika kipindi  cha miaka mitatu cha Serikali ya Awamu ya Tano, viwanda 3600 vimesajiliwa na viwanda vingi kati ya hivyo vikiwa  katika  mkoa wa Pwani.

Ameendelea  kusema, tangu kiwanda  hicho kianze kufanya kazi Agosti, 2018 jumla ya Watanzania 450 wamepata ajira na wengine wakiendelea kuajiriwa kadri kiwanda kinavyoendelea kuzalisha.

Vilevile amesema, kiwanda hicho kimetoa ajira kwa wakulima wa matunda, ambao huuza matunda yao moja kwa moja kiwandani. Pia kiwanda kimekuwa suluhisho kubwa la kupatikana kwa soko la matunda nchini badala ya kuachwa na kuharibika mashambani.

[caption id="attachment_40161" align="aligncenter" width="900"] Maembe yakiwa katika makasha maalum katika Kiwanda cha kuzalisha juisi cha Sayona kilichopo Chalinze mkoani Pwani. Kujengwa kwa kiwanda hicho ni matokeo ya dhana ya ujenzi wa viwanda inayosisitizwa na Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais, Dkt John Pombe Magufuli.[/caption]

“Nchi nyingi za Afrika matunda yamekuwa yakiharibika njiani au mashambani. Lakini sisi  tunawapa  elimu wakulima  wa  matunda  namna ya kuyatunza matunda hayo ili yaweze kufika kiwandani yakiwa hayajaharibika,” amesema Patel.

Kwa upande wake, mkulima wa matunda  ya maembe kutoka Handeni, Tanga, Mbwali Chewe amesema, soko la matunda ya maembe lilikuwa gumu katika kipindi cha miaka ya nyuma, kutokana na kutokuwa na soko la uhakika.

“Ujio wa kiwanda cha Sayona ni faraja kubwa kwetu  wakulima wa matunda nchini, kwani sasa tunasoko la uhakika la kuuza matunda. Nimekuja na lori 6 za maembe kutoka Handeni ninategemea kupata milioni 2,” amesema Chewe.

Nae, Mtunza Stoo na Mtoa Mizigo wa Kiwanda hicho, Khadija Ngoka ambaye ni mzaliwa wa mkoa wa Pwani amesema uwepo wa kiwanda hicho umesaidia kutoa ajira kwa watu wa aina zote, waliokuwa na elimu na wasiokuwa na elimu, wazee na vijana bila kubagua jinsia, dini au kabila.

“Kiwanda cha Sayona, hapa Chalinze kimepunguza kwa kiwango kikubwa idadi ya watoto wa mitaani, kutokana na wengi wao kwa sasa wanapata ajira mbalimbali kama za ulinzi, usafi na vibarua hapa kiwandani,” amesema Khadija.

Kiwanda  cha Sayona mkoani Pwani kiliwekwa jiwe la msingi na Mhe. Rais Dkt. John Pombe Magufuli Juni 2017 na kimeanza kufanya kazi Agosti 2018. Ujenzi wa kiwanda hicho umegharimu dola za kimarekani Milioni 55 ambapo kimejikita katika uzalishaji wa juisi za matunda ya Embe, Pasheni, Pera, Chungwa na Nanasi.

[caption id="attachment_40153" align="aligncenter" width="900"] Wafanyakazi wa kiwanda cha kuzalisha juisi cha Sayona kilichopo Chalinze mkoani Pwani wakiwa kazini.[/caption]

Tangu kiwanda kianze uzalishaji kimeshanunua matunda mbalimbali kutoka   Njombe, Kahama, Tanga, Shinyanga, Tabora, na Pwani.

Aidha, kiwanda kimekuwa kikichangia huduma mbalimbali za jamii kwa wananchi wanao zunguka kiwanda, kama vile kutoa huduma ya gari la wagonjwa, gari la zimamoto pamoja na hospitali iliyopo ndani ya kiwanda hicho. Pia imechangia ununuzi wa madawati kwa shule za msingi na sekondari pamoja na vifaa vya mahospitalini katika mkoa wa Pwani.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi