[caption id="attachment_38078" align="aligncenter" width="750"] Rais John Pombe Magufuli na mkewe Mama Janeth Magufuli wakishiriki katika Misa ya Shukurani ya Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu Mhe.Benjamin William Mkapa kutimiza umri wa miaka 80 katika kanisa la Mtakatifu Imakulata jijini Dar es salaam leo Novemba 12, 2018.Kulia kwa Mhe. Mkapa ni mkewe Mama Anna Mkapa[/caption]
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli amempongeza Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu Mhe. Benjamin William Mkapa kwa mchango wake mkubwa alioutoa wakati wa uongozi wake.
Mhe. Rais Magufuli ametoa pongezi hizo katika Misa Takatifu ya Shukrani ya Uhai kwa Rais Mstaafu Mkapa ambaye leo tarehe 12 Novemba, 2018 ametimiza miaka 80 tangu kuzaliwa iliyofanyika katika Parokia ya Bikira Maria Imakulata, Upanga Jijini Dar es Salaam na kuongozwa na Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo.
Mhe. Rais Magufuli amesema wakati akiwa madarakani Rais Mstaafu Mkapa amefanya mambo mengi na muhimu kwa Taifa na amebainisha kuwa Watanzania wataendelea kumkumbuka kwa kazi nzuri aliyoifanya.
[caption id="attachment_38079" align="aligncenter" width="750"] Rais John Pombe Magufuli na mkewe Mama Janeth Magufuli wakimpa zawadi ya kadi na kisha kumpongeza Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu Mhe.Benjamin William Mkapa akiwa na mkewe Mama Anna Mkapa kwa kutimiza umri wa miaka 80 katika Misa ya Shukurani ya uhai iliyofanyika katika kanisa la Mtakatifu Imakulata jijini Dar es salaam leo Novemba 12, 2018[/caption]“Mhe. Rais Mstaafu Mkapa wakati wa uongozi wako ulifanya kazi kubwa, na kwa miaka 20 ambayo nilifanya kazi na wewe baada ya kuniteua kuwa Naibu Waziri na baadaye Waziri nilijifunza kuwa wewe ni mcha Mungu, muadilifu, mnyenyekevu kwa Mungu na mchapakazi.
“Leo unapotimiza miaka 80 na kushukuru na kukupongeza sana, na kuombea Mwenyezi Mungu aendelee kukupa afya njema wewe na familia yako, na sisi viongozi tuliopo sasa tutaendelea kuyaenzi mazuri yote uliyoyafanya” amesemaMhe. Rais Magufuli.
Kwaupande wake Mhe. Rais Mstaafu Mkapa amemshukuru Mhe.Rais Magufuli kwa kumtakia heri, amewashukuru Maaskofu Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo, Askofu Mkuu Mwandamizi Jude Thadaeus Ruwai’china Askofu Msaidizi Eusebius Nzigirwa walioongozaMisa hiyo pamoja na viongozi wengine na waumini wenzake.
Rais Mstaafu Mkapa amebainisha kuwa anampongeza Mhe.Rais Magufuli kwa uongozi wake kwakuwa Tanzania imeendelea kuwa na sifa nzuri ya amani na umoja na kwamba hata akiwa nje ya nchi anapoulizwa siri ya Tanzania kuwa na Marais Wastaafu watatu ambao wanaishi vizuri nchini mwao, huwajibu kuwa siri kubwa ni uwepo wa amani, umoja na mshikamano.
[caption id="attachment_38080" align="aligncenter" width="750"] Rais John Pombe Magufuli na mkewe Mama Janeth Magufuli wakiongea kwa furaha na Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu Mhe. Benjamin William Mkapa na mkewe Mama Anna Mkapa baada ya Misa ya Shukurani kwa Mhe. Mkapa kutimiza umri wa miaka 80 katika kanisa la Mtakatifu Imakulata jijini Dar es salaam leo Novemba 12, 2018[/caption] [caption id="attachment_38081" align="aligncenter" width="750"] Rais John Pombe Magufuli na mkewe Mama Janeth Magufuli wakiwa katika picha ya pamoja Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu Mhe. Benjamin William Mkapa na mkewe Mama Anna Mkapa pamoja na Maaskofu wakati wa Misa ya Shukrani kwa Mhe. Mkapa kutimiza umri wa miaka 80 katika kanisa la Mtakatifu Imakulata jijini Dar es salaam leo Novemba 12, 2018[/caption]Misa hiyo imehudhuriwa na Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli na Mke wa Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu Mama Anna Mkapa.
Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam
12 Novemba, 2018