Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Rais Magufuli Atengua Uteuzi wa Profesa Muhongo
May 24, 2017
Na Msemaji Mkuu

[caption id="attachment_1479" align="aligncenter" width="750"] Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza wakati wa hafla ya kupokea ripoti ya kamati ya kwanza ya iliyoiunda kwa ajili ya kuchunguza kiwango cha madini kilichopo kwenye mchanga wa madini (Makinikia) uliokamatwa katika bandari ya Dar es Salaam ukiwa katika makontena 277 tayari kwa kusafirishwa nje ya nchi. Kutoka kulia ni Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu Hassan na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Mhandisi John Kijazi.[/caption]

Na Jacquiline Mrisho.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli ametengua uteuzi wa Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo muda mfupi baada ya kupokea ripoti ya Kamati ya kuchunguza mchanga wa madini (makinikia) uliomo kwenye makontena yaliyozuiliwa na Serikali kusafirishwa nje ya nchi.

Taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi John Kijazi imeeleza kuwa nafasi ya Waziri wa Nishati na Madini itajazwa baadae.

Mapema asubuhi baada ya kupokea ripoti hiyo iliyoonesha mchanga uliokuwa unachunguzwa ulikuwa na wastani wa kiasi cha thamani kati ya shilingi bilioni 829.4 kwa kutumia viwango vya wastani wa chini na trilioni 1.439 kwa kutumia viwango vya juu.

[caption id="attachment_1480" align="aligncenter" width="750"] Mwenyekiti wa Kamati ya kwanza ya Wataalam wa Jiolojia iliyoiundwa kwa ajili ya kuchunguza kiwango na aina ya madini yaliyopo kwenye mchanga wa madini (Makinikia), Profesa Abdulkarim Hamis Mruma akiwasilisha ripoti yao mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli (hayupo pichani) wakati hafla ya kuwasilisha ripoti hiyo Ikulu jijini Dar es Salaam leo. Kamati hiyo ya watu wanane iliundwa kufuatia kukamatwa kwa makontena 277 yakiwa na mchanga huo katika bandari ya Dar es Salaam tayari kwa kusafirishwa nje ya nchi. Kutoka kulia ni Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu Hassan na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Mhandisi John Kijazi.[/caption] [caption id="attachment_1481" align="aligncenter" width="632"] Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipokea ripoti kutoka kwa Mwenyekiti wa Kamati ya kwanza ya Wataalam wa Jiolojia iliyoiundwa kwa ajili ya kuchunguza kiwango na aina ya madini yaliyopo kwenye mchanga wa madini (Makinikia), Profesa Abdulmalik Mruma katika hafla iliyofanyika leo Ikulu Jijini Dar es Salaam. Kamati hiyo iliundwa kufuatia kukamatwa kwa makontena 277 yakiwa na mchanga huo katika bandari ya Dar es Salaam tayari kwa kusafirishwa nje ya nchi. Katikati ni Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu Hassan.[/caption]

Kufuatia taarifa hiyo Rais Magufuli aliivunja Bodi ya Wakala wa Ukaguzi wa Madini Tanzania (TMAA) na kumsimamisha kazi Mtendaji Mkuu wa Wakala hiyo kutokana na kutosimamia ipasavyo mchakato mzima wa usafirishaji mchanga wenye madini nje ya nchi na hivyo kuisababishia nchi hasara kubwa.

“Nawapongeza Kamati kwa ripoti mliyoiwasilisha ambayo inasikitisha na ripoti hii haiwezi kupita hivi hivi kwani tutaonekana watu wa ajabu. Hivyo kuanzia sasa nimeivunja rasmi Bodi ya Wakala wa Ukaguzi wa Madini (TMAA), nimemsimamisha kazi Afisa Mtendaji Mkuu wa TMAA pia  namtaka Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo ambaye ni rafiki yangu lakini kwenye hili ningependa ajifikirie na achukue hatua ya kujiuzuru”, alieleza Rais Magufuli kabla ya kutengua uteuzi wa Waziri Muhongo.

Mbali na kutengua uteuzi wa Waziri wa Nishati, kuvunja Bodi ya Wakurugenzi na kumsimamisha kazi Mtendaji Mkuu wa TMAA, Dkt. Magufli pia amevitaka vyombo vya dola kuwachunguza na kuwachukulia hatua watendaji wa Wizara ya Nishati na Madini na wafanyakzi wote waliohusika na kushindwa kusimamia vema mchakato mzima wa usafirishaji wa mchanga wenye madini nje ya nchi.

[caption id="attachment_1482" align="aligncenter" width="750"] Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipitia ripoti ya Kamati ya kwanza ya Wataalam wa Jiolojia iliyoiundwa kwa ajili ya kuchunguza kiwango na aina ya madini yaliyopo kwenye mchanga wa madini (Makinikia) mara baada ya kukabidhiwa na Mwenyekiti wa Kamati hiyo Profesa AbdulKarim Hamis Mruma (kushoto) katika hafla iliyofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam leo. Kamati hiyo iliundwa kufuatia kukamatwa kwa makontena 277 yakiwa na mchanga huo katika bandari ya Dar es Salaam tayari kwa kusafirishwa nje ya nchi. Kutoka kulia ni Wazri Mkuu Kassim Majaliwa na Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu Hassan (watatu kutoka kulia).[/caption] [caption id="attachment_1483" align="aligncenter" width="750"] Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipata ufafanuzi kutoka kwa Mwenyekiti wa Kamati ya kwanza ya Wataalam wa Jiolojia iliyoiundwa kwa ajili ya kuchunguza kiwango na aina ya madini yaliyopo kwenye mchanga wa madini (Makinikia), Profesa Abdulkarim Hamis Mruma kuhusu baadhi ya takwimu zilizopo katika ripoti ya Kamati ya kwanza ya Wataalam wa Jiolojia iliyoiundwa kwa ajili ya kuchunguza kiwango na aina ya madini yaliyopo kwenye mchanga wa madini (Makinikia) mara baada ya kukabidhiwa na Mwenyekiti huyo Ikulu Jijini Dar es Salaam leo. Kamati hiyo iliundwa kufuatia kukamatwa kwa makontena 277 yakiwa na mchanga huo katika bandari ya Dar es Salaam tayari kwa kusafirishwa nje ya nchi. Kululia ni Wazri Mkuu Kassim Majaliwa.[/caption] [caption id="attachment_1486" align="aligncenter" width="750"] Wajumbe wa Kamati ya Kwanza ya Wataalam wa Jiolojia iliyoiundwa kwa ajili ya kuchunguza kiwango na aina ya madini yaliyopo kwenye mchanga wa madini (Makinikia) wakiwa tayari kwa kuwasilisha ripoti yao katika hafla iliyofanyika Ikulu leo Jijini Dar es Salaam. Kamati hiyo iliundwa tarehe 29 Machi 2017, kufuatia kukamatwa kwa makontena 277 yakiwa na mchanga huo katika bandari ya Dar es Salaam tayari kwa kusafirishwa nje ya nchi. Wajumbe wa Kamati hiyo iliyoongozwa na Mwenyekiti wake Profesa Abdulkarim Hamis Mruma, wengine ni Profesa Justianian Rwezaura Ikingula, Profesa Joseph Bushweshaiga, Dk Yusuf Ngenya, Dk Joseph Yoweza Philip, Dk Ambrose Itika, Mohamed Zengo Makongoro na Hery Issa Gombela.[/caption] [caption id="attachment_1489" align="aligncenter" width="750"] Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam akisalimiana na Viongozi wa Vyama vya Siasa alipokutana nao katika hafla ya kukabidhi ripoti ya Kamati ya kwanza ya Wataalam wa Jiolojia iliyoiundwa kwa ajili ya kuchunguza kiwango na aina ya madini yaliyopo kwenye mchanga wa madini (Makinikia) Ikulu Jijini Dar es Salam leo.[/caption] [caption id="attachment_1492" align="aligncenter" width="750"] Mkuu wa Jeshi la Ulinzi Tanzania – JWTZ, (CDF) Venance Mabeyo akiteta jambo na Mwanasheria Mkuu wa Serikali Jaji George Masaju alipokutana nao katika hafla ya kukabidhi ripoti ya Kamati ya kwanza ya Wataalam wa Jiolojia iliyoiundwa kwa ajili ya kuchunguza kiwango na aina ya madini yaliyopo kwenye mchanga wa madini (Makinikia) Ikulu Jijini Dar es Salam leo. Kamati hiyo iliundwa tarehe 29 Machi 2017, kufuatia kukamatwa kwa makontena 277 yakiwa na mchanga huo katika bandari ya Dar es Salaam tayari kwa kusafirishwa nje ya nchi.[/caption] [caption id="attachment_1493" align="aligncenter" width="750"] Wasanii wa Kundi la Tanzania All Stars wakitumbuiza wimbo wa kuhamasisha uzalendo wakati wa hafla ya kukabidhi ripoti ya Kamati ya kwanza ya Wataalam wa Jiolojia iliyoiundwa kwa ajili ya kuchunguza kiwango na aina ya madini yaliyopo kwenye mchanga wa madini (Makinikia) Ikulu Jijini Dar es Salam leo. Kamati hiyo iliundwa tarehe 29 Machi 2017, kufuatia kukamatwa kwa makontena 277 yakiwa na mchanga huo katika bandari ya Dar es Salaam tayari kwa kusafirishwa nje ya nchi.[/caption] [caption id="attachment_1494" align="aligncenter" width="750"] Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Joseph Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa Kamati ya Kamati ya kwanza ya Wataalam wa Jiolojia iliyoiundwa kwa ajili ya kuchunguza kiwango na aina ya madini yaliyopo kwenye mchanga wa madini (Makinikia) Ikulu Jijini Dar es Salam leo. Kamati hiyo iliundwa tarehe 29 Machi 2017, kufuatia kukamatwa kwa makontena 277 yakiwa na mchanga huo katika bandari ya Dar es Salaam tayari kwa kusafirishwa nje ya nchi.(Picha na: Frank Shija).[/caption]

Akifafanua taarifa ya ripoti hiyo, Mwenyekiti wa Kamati ya Uchunguzi wa Mchanga wa Madini, Prof. Abdulkarim Mruma amesema kuwa katika uchunguzi huo wamebaini kuwa kuna viwango vikubwa vya madini yanayojulikana pamoja na aina zingine za madini yasizojulikana ambayo ni muhimu na ya gharama ambayo yalikuwa yakichukuliwa bila kuhesabiwa.

“Tumeyafanyia uchunguzi jumla ya makontena 277 ambayo yalizuiliwa kusafirishwa na Mhe. Rais Magufuli kwa ajili ya kufanyiwa uchunguzi wa kina hivyo katika uchunguzi wetu tumegundua kuwa makontena 277 yenye madini ya kawaida pamoja madini ya kimkakati thamani yake ni wastani wa bilioni 829.4 hadi trilioni 1.439”, alisema Prof. Mruma.

Prof. Mruma ameongeza kuwa Kamati hiyo imebaini ukosefu wa vifaa vya kukagulia (scanner) vitu vilivyomo kwenye makontena hayo kwani baada ya kufanya ukaguzi vifaa hivyo havikuonyesha vitu vilivyomo ndani.

Machi 29 mwaka huu, Rais Magufuli aliunda Kamati ya kwanza ya watu nane ikiongozwa na Profesa Abdulrahim Mruma kuchunguza makontena 277 yenye mchanga uliokuwa usafirishwe nje ya nchi.

   

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi