Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Rais Magufuli Afanya Ziara ya Kushtukiza Kukagua Kazi ya Upakaji wa Rangi Ndege ya Foker 50
Mar 28, 2019
Na Msemaji Mkuu

[caption id="attachment_41484" align="aligncenter" width="1000"] Sehemu ya ndani na nje ya Ndege hiyo ya Foker 50 ambayo kazi ya ufungaji wa viti vipya kutoka 32-48 umekamilika na kazi ya upakaji wa rangi ikielekea ukingoni. Hapo awali ndege hiyo ilikuwa iende nje ya nchi kwa ajili ya kupaka rangi na kuchora ndembo ya twiga kwa gharama zaidi ya Shilingi milioni 160 kabla ya Rais Dkt. Magufuli kutoa maagizo kazi hiyo ifanyike nchini na mafundi wa ATCL ambapo gharama yake ni Shilingi Milioni 7.[/caption] [caption id="attachment_41485" align="aligncenter" width="750"] Muonekana wa ndege ya Foker 50 ambayo kazi ya ufungaji wa viti vipya kutoka 32-48 umekamilika na kazi ya upakaji wa rangi ikielekea ukingoni. [/caption] [caption id="attachment_41486" align="aligncenter" width="1000"] Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo na Mafundi wazalendo ambao wamefanya kazi ya kuandika na kuchora nembo ya Twiga pamoja na kupaka rangi ndege hiyo ya Foker 50 kwa gharama ya Shilingi milioni 7. Pia Rais Dkt. Magufuli amewazawadia mafundi hao kiasi cha Shilingi milioni 10 kutokana na kazi yao nzuri ya kizalendo walioifanya.[/caption] [caption id="attachment_41487" align="aligncenter" width="1000"] Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Mkurugenzi wa ATCL Ladislaus Matindi wakati wa Ukaguzi wa ndege hiyo aina ya Foker 50[/caption] [caption id="attachment_41488" align="aligncenter" width="1000"] Sehemu ya Ndani na nje ya Ndege hiyo ya Foker 50 ambayo kazi ya ufungaji wa viti vipya kutoka 32-48 umekamilika na kazi ya upakaji wa rangi ikielekea ukingoni. Hapo awali ndege hiyo ilikuwa iende nje ya nchi kwa ajili ya kupaka rangi na kuchora ndembo ya twiga kwa gharama zaidi ya Shilingi milioni 160 kabla ya Rais Dkt. Magufuli kutoa maagizo kazi hiyo ifanyike nchini na mafundi wa ATCL ambapo gharama yake ni Shilingi Milioni 7.[/caption] [caption id="attachment_41489" align="aligncenter" width="1000"] Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akikagua ndege aina ya Foker 50 iliyokuwa ikitumika kubeba Viongozi wa Serikali na sasa itatumika kubeba abiria wa kawaida katika mikoa mbalimbali hapa nchini. Rais Dkt. Magufuli alizuia ndege hiyo kusafirishwa nje ya nchi kwa ajili ya kazi hiyo ambapo ingegharimu zaidi ya Shilingi milioni 160 wakati kazi hiyo imefanywa na mafundi wa ndani kwa gharama ya shilingi Milioni 7.[/caption]

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi