Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Rais Magufuli Aahidi Kuiunganisha Kanda ya Kusini Kiuchumi
Apr 03, 2019
Na Msemaji Mkuu

[caption id="attachment_41665" align="aligncenter" width="750"] Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Mkewe Mama Janeth Magufuli pamoja na Viongozi wengine wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mkoa wa Mtwara, Wabunge na viongozi wengine akivuta utepe kuweka jiwe la msingi katika ujenzi wa Barabara ya Mtwara-Newala-Masasi km 210 sehemu ya Mtwara-Mnivata km 50 katika hafla iliyofanyika sehemu ya Naliendelea mkoani Mtwara.[/caption]

Na. Paschal Dotto-MAELEZO

Rais Dkt John Pombe Magufuli amewahakikishia wananchi wa Nanyamba, Tandahimba, na Newala Mkoani Mtwara kuwa Serikali itaendelea kuimarisha miundombinu ya uhakika ili kuunganisha Kanda ya Kusini Kiuchumi na wananchi wa Mkoa huo kuendelea kufanya kazi kwa juhudi ili kuweza kujiletea maendeleo yao.

Akizungumza katika maeneo mbalimbali ya Mkoa huo, Rais Magufuli amesema Serikali itaanza ujenzi wa barabara ya Mtwara-Tandahimba-Nanyamba yenye urefu wa kilometa 50 itakayogharimu kiasi cha Tsh.bilioni 86 na kumwagiza Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Isack Kamwelwe kutangaza zabuni ya ujenzi wa kilometa zingine na kufikia kilometa 100 na hivyo kuunganisha kwa urahisi nyanda za kiuchumi katika mikoa ya kusini.

“Barabara hii itakuwa ni kiunganishi cha uchumi mikoa ya kusini, hatuwezi kushindwa kujenga kilometa 100, lengo letu kuu ni kuiunganisha Bandari yetu ya Mtwara na mizigo inayotoa Malawi,” alisema Rais Magufuli.

Aidha Rais Magufuli alisema kuwa katika kuwainua wakulima wa Mkoa wa Mtwara, ambapo Serikali imetekeleza ununuzi wa korosho kutoka kwa wananchi wenye korosho zaidi ya kilo 1500, na Tsh Bilioni 50 tayari zimetengwa kwa ajili ya kuwalipa wakulima hao, na kwa upande wa wakulima wa korosho wenye kilo chini ya 1500 wamelipwa kiasi cha Tsh Bilioni 578.

Rais Magufuli amewahiza wafanyabiashara walanguzi wa zao la korosho ‘Kagomba’ kuacha kuwadhulumu wakulima wadogo kwa kuwapa bei ambayo hailidhishi huku wakijua wametumia gharama kubwa katika kuendeleza zao hilo, na kusema serikali ya Awamu ya tano haitarudi nyuma kuwatetea wakulima hao.

“Utakuta mtu amelima korosho zake, amenunua madawa, ametumia gharama kuzivuna unakuja kumpa bei ya 1500, kwa Serikali ya Awamu ya Tano hili halikubaliki”, alisema Rais Magufuli.

Akiongelea miradi mingine inayotekelezwa serikali ya Awamu ya Tano kuwa ni pamoja na upanuzi wa bandari ya Mtwara, , upanuzi wa uwanja wa Ndege na ukarabari wa mradi wa maji wa makonde ambao utagharimu kiasi cha Tsh.bilioni 160 zikiwa ni fedha za mikopo kutoka Serikali ya India unaowezesha ujenzi wa miradi ya maji katika miji 28 nchini..

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi