Rais Dkt. Mwinyi Azindua Ripoti ya Mahitaji ya Mahkama Zanzibar na Uzinduzi wa Ofisi za Watetezi wa Haki za Binadamu Zanzibar
Sep 17, 2022
Na
Jacquiline Mrisho
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi akizindua Kitabu cha Ripoti ya Mahitaji ya Mfumo wa Mahakama Zanzibar, hafla hiyo ya uzinduzi iliyofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Golden Tulip Uwanja wa Ndege Kiembesamaki Wilaya ya Magharibi “B” Unguja, leo 17-9-2022, na (kushoto kwa Rais) Jaji Mkuu wa Zanzibar Khamis Ramadhan Shaban na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Katiba,Sheria,Utumishi na Utawala Bora Zanzibar Mhe. Haroun Ali Suleiman na (kulia kwa Rais) Mratibu wa Kitaifa Wakili Onesmo Olengurumwa
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi akionesha Kitabu cha Ripoti ya Mahitaji ya Mfumo wa Mahakama Zanzibar, baada ya kuizindua rasmi leo tarehe 17-9-2022, katika ukumbi wa Hoteli ya Golden Tulip Uwanja wa Ndege Kiembesamaki Wilaya ya Magharibi “B” Unguja na (kushoto kwa Rais) ni Jaji Mkuu wa Zanzibar, Khamis Ramadhan Shaban na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Katiba,Sheria, Utumishi na Utawala Bora Zanzibar, Mhe. Dkt. Haroun Ali Suleiman na (kulia kwa Rais) ni Mratibu wa Kitaifa, Wakili Onesmo Olengurumwa.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi akihutubia katika hafla ya Uzinduzi wa Ripoti ya Mahitaji ya Mfumo wa Mahakama Zanzibar na Uzinduzi wa Ofisi ya Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Zanzibar, uzinduzi huo uliyofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Golden Tulip Uwanja wa Ndege Kiembesamaki Wilaya ya Magharibi “B” Unguja leo 17-9-2022.
Washiriki wa uzinduzi wa Ripoti ya Mahitaji ya Mfumo wa Mahakama Zanzibar na uzinduzi wa Ofisi Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Zanzibar wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi akihutubia katika hafla hiyo iliyofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Golden Tulip Uwanja wa Ndege Kiembesamaki Wilaya ya “B” Unguja leo tarehe 17-9-2022.