Rais Dkt. Mwinyi Ashuhudia Utiaji Saini Makabidhiano ya "Data" za Utafutaji wa Mafuta na Gesi Asilia Zanzibar.
Aug 10, 2022
Na
Jacquiline Mrisho
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi akishuhudia utiaji saini makabidhiano ya “DATA” za Utafutaji wa Mafuta na Gesi Asilia kwa Vitalu vya Zanzibar, wakisaini makabidhiano hayo (kulia kwa Rais) ni Waziri wa Nishati wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Januari Yussuf Makamba na (kushoto kwa Rais) ni Waziri wa Uchumi wa Buluu na Uvuvi Zanzibar, Mhe Suleiman Masoud Makame, hafla hiyo ilifanyika katika viwanja vya Ikulu Jijini Zanzibar leo 10-8-2022.(
Waziri wa Nishati wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Januari Yussuf Makamba akimkabidhi "DATA" za Utafutaji wa Mafuta na Gesi Asili kwa Vitalu vya Zanzibar, Waziri wa Uchumi wa Buluu na Uvuvi Zanzibar, Mhe. Suleiman Masoud Makame. (kulia) wakati wa hafla ya utiaji saini. Makabidhiano hayo yalifanyika katika viwanja vya Ikulu Jijini Zanzibar leo 10-8-2022, na kushuhudiwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi.
Wakuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama Zanzibar wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi (hayupo pichani) akizungumza katika hafla ya Utiaji Saini makabidhiano ya “DATA” za Utafutaji wa Mafuta na Gesi Asilia kwa Vitalu vya Zanzibar, hafla iliyofanyika katika viwanja vya Ikulu Jijini Zanzibar leo 10-8-2022.
Baadhi ya Mawaziri wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar wakifuatilia Utiaji wa Saini ya Makabidhiano ya “DATA” za Utafutaji wa Mafuta na Gesi Asilia kwa Vitalu vya Zanzibar, wakati Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi.(hayupo pichani) akizungumza katika hafla hiyo iliyofanyika katika viwanja vya Ikulu Jijini Zanzibar leo 10-8-2022.
Baadhi ya Watendaji wa SMT na SMZ wakifuatilia Utiaji Saini wa Makabidhiano ya “DATA” za Utafutaji wa Mafuta na Gesi Asilia kwa Vitalu vya Zanzibar, makabidhiano yaliyofanyika katika viwanja vya Ikulu Jijini Zanzibar leo 10-8-2022, wakati Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi (hayupo pichani) akizungumza baada ya utiaji wa saini hafla iliyofanyika katika viwanja vya Ikulu Jijini Zanzibar.