Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Rais Dkt. Mwinyi Amekutana na Ujumbe wa Jumuiya ya Mabunge ya Canada -Afrika Ikulu Zanzibar
Feb 22, 2024
Rais Dkt. Mwinyi Amekutana na Ujumbe wa Jumuiya ya Mabunge ya Canada -Afrika Ikulu Zanzibar
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi akisalimiana na mgeni wake Balozi wa Canada Nchini Tanzania, Mhe. Kyle Nunas, alipofika Ikulu Jijini Zanzibar na Ujumbe wa Jumuiya ya Mabunge ya Canada-Afrika kwa mazungumzo yaliyofanyika katika ukumbi wa Ikulu Zanzibar leo 22-2-2024.
Na Ikulu - Zanzibar

Ujumbe wa Jumuiya ya Mabunge ya Canada – Afrika wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi wakati wa mazungumzo yao yaliyofanyika katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar leo 22-2-2024, ujumbe huo uliongozwa na Balozi wa Canada Nchini Tanzania, Mhe. Kyle Nunas na (kulia kwake) ni Kiongozi wa Ujumbe huo, Seneta Mhe. Amina Gerba.

 

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi akikabidhiwa zawadi maalum na Kiongozi wa Ujumbe wa Jumuiya ya Mabunge ya Canada-Afrika, Seneta Amina Gerba na (kulia kwake) Mhe. Brenda Shanahan, baada ya kumalizika kwa mazungumzo yao yaliyofanyika katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar leo 22-2-2024

 

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi  akizungumza na kubadilishana mawazo na Ujumbe wa Jumuiya ya Mabunge ya Canada –Afrika, baada ya kumaliza mazungumzo yao yaliyofanyika katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar leo 22-2-2024.

 

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi